ARUSHA NAKO YALE YALE:TRA YAWATAKA WAFANYABIASHARA KUFUNGUA MADUKA YAO NA KUACHA KUENDELEA KUGOMEA MASHINE ZA EFDS
Na Pamela Mollel,Arusha
Wafanyabiashara
hapa nchi wametakiwa kutoendeleza mgomo wa mashine za kieletroniki za
EFD’S na badala yake wafungue maduka na kuendelea na biashara zao kwa
kutumia mashine kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza masharti ya
kufanyabiashara.
Rai
hiyo aliitoa jana Kaimu kamishna mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania
Rished Bade wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha ambapo
alisema kuwa kitendo cha kutumia mashine kwa wafanyabiashara
itawawezesha kuweka kumbukumbu sahihi.
Alisema
kuwa kodi ya ongezeko la dhamani ilikuwa kwenye awamu ya kwanza hivyo
awamu ya pili wafanyabiashara hawatahusika kulipa kodi kama wengine
wanavyodai
“siyo
kweli kwamba wakitumia mashine watafilisika bali watakuwa na kumbukumbu
sahihi…na kuna watu wachache wanapotosha wafanyabiashara kwa hili”
alisema Bade.
Aidha
aliwataka wafanyabiashara kutokubali kutumika na wasiowafanyabiashara
ambao wamekuwa wakiwashawishi kufunga maduka ili kushinikiza serikali
bali wawaripoti katika mamlaka husika ili sheria ichukue mkondo wake
Post a Comment