VUMBI LIGI KUU KUTIMKA WIKIENDI
Mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa
Tanzania Bara unaanza kesho (Januari 25 mwaka huu) kwa mechi nne
zitakazochezwa katika miji ya Bukoba, Dar es Salaam na Tanga.
Mabingwa watetezi Yanga watakuwa wageni wa Ashanti United kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati kwenye jiji hilo hilo Uwanja wa
Azam Complex kutakuwa na mechi kati ya wenyeji Azam FC na Mtibwa Sugar
kutoka Morogoro.
Coastal Union na Oljoro JKT zitaumana kwenye Uwanja wa Mkwakwani
jijini Tanga, huku Kagera Sugar ikiikaribisha Mbeya City kwenye Uwanja
wa Kaitaba mjini Bukoba.
Raundi ya 14 ya ligi hiyo itaendelea Jumapili (Januari 26 mwaka huu)
kwa mechi mbili. Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam utakuwa shuhuda wa mechi
kati ya Simba na Rhino Rangers kutoka Tabora wakati maafande wa JKT
Ruvu na Mgambo Shooting watapambana Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es
Salaam.
Viingilio kwenye mechi ya Ashanti United na Yanga vitakuwa sh. 5,000,
sh. 15,000 na sh. 20,000. Viingilio mechi ya Mkwakwani vitakuwa sh.
10,000 kwa sh. 3,000, Uwanja wa Azam Complex sh. 10,000 kwa sh. 3,000,
Uwanja wa Kaitaba ni sh. 5,000 kwa sh. 3,000.
Post a Comment