Niyonzima, Cannavaro wataka kuchapana makonde uwanjani
WACHEZAJI wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na
Haruna Niyonzima, juzi Jumatano almanusura wachapane makonde uwanjani
wakati wa mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Coastal Union kwenye
Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa.
Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili cha mchezo huo baada ya Cannavaro kutaka kujifunga alipokuwa kwenye harakati za kuokoa hatari langoni kwake, ndipo Niyonzima akakasirishwa na kitendo hicho.
Mara baada ya Cannavaro kuokoa ndipo Niyonzima akamvaa akimlaumu, kuona hivyo Cannavaro naye akaja juu, ndipo wawili hao walipoanza kuzozana, huku kila mmoja akionekana kupandwa na jazba.
Baada ya kuvutana kwa sekunde kadhaa ndipo kila mmoja akarudi kwenye nafasi yake kuendelea na majukumu lakini wote wakiwa wamekunja ndita.
Alipoulizwa juu mara baada ya kipenga cha mwisho, Cannavaro alisema: “Hakuna mwenye chuki na mwenzake, kilichotokea ni kawaida kwenye soka, japo tulikasirishana kiukweli.”

Post a Comment