MAJANGA MAN UTD: MANCHESTER UNITED YAONDOLEWA CAPITAL ONE CUP KWA MATUTA
Shangwe: Wachezaji wa Sunderland wakishangilia kutinga fainali baada ya kuwaondoa Man Utd.
TIMU ya Manchester United imeendelea kusuasua katika michuano mbalimbali baada ya kuondolewa na Sunderland katika nusu fainali za michuano ya Kombe la Ligi maarufu kama Capital One Cup iliyopigwa Old Trafford.
Manchester imetupwa nje ya mashindano hayo kwa mikwaju ya penalti baada ya matokeo ya awali kuwa sare ya 3-3 na Sunderland kushinda kwa penalti 2-1.
Baada ya matokeo hayo, Sunderland inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi 18 juu ya Cardiff City katika Ligi Kuu ya England, itakutana na Manchester City Machi 2 mwaka huu katika fainali itakayopigwa uwanja wa Wembley.

Post a Comment