ad

ad

Logarusic: Rage alitakiwa kuniuliza mimi

KOCHA Mkuu wa Simba, Mcroatia, Zdravko Logarusic, amesema hatafanya kazi na kocha   Mganda, Amatre Richard, kwa kuwa hajahusishwa kwenye uteuzi wake.
Tayari imebainika kuwa Mganda huyo ameshatua nchini, akidaiwa kuletwa na mwenyekiti wa timu hiyo, Ismail Aden Rage, ambaye alionyesha hofu ya kuteuliwa kwa Selemani Matola huku akitaka arejeshwe kikosi cha vijana.

Akizungumza na Logarusic ‘Loga’, alisema katika uteuzi wa kocha msaidizi, lazima kocha mkuu ahusike kwani yeye ndiye mwenye uwezo wa kujua mtu atakayemfaa kwenye benchi la ufundi.

Aliongeza kuwa, kabla ya kutua Simba, aliomba mapema kufahamishwa sifa za msaidizi wake na kuridhika na utendaji wa Matola, hivyo hayupo tayari kufanya kazi na kocha mwingine zaidi ya Matola.
“Kwangu mpaka sasa sijui chohote, lakini kama ni hivyo walitakiwa kuniambia mimi, kiheshima mwenyekiti alitakiwa kunifuata na kunieleza.

“Niseme ukweli kama kweli ndiyo hivyo mimi sipo tayari kufanya kazi na kocha huyo, ninachotaka mimi ni kuendelea kufanya kazi na Matola kwa kuwa tunaelewana na sifa zake nilizikubali tangu awali,” alisema Loga.

Amatre yupo hapa nchini na inaelezwa kuwa ameletwa na Rage kwa kuwa awali kocha huyo alikuwa kwenye benchi la ufundi la Simba lakini hakumaliziwa fedha zake za mshahara, hivyo anatakiwa kufanya kazi ili amalizie mkataba wake.
Powered by Blogger.