LIVERPOOL INATISHA, YAWAFUMUA EVERTON 4-0
LIVERPOOL
imefanya kufuru baada ya kuwafumua mabao 4-0 wapinzani wao, Everton
katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Anfileld.
Mabao ya Liverpool yamefungwa na Steven Gerrard dakika ya 21, Daniel Sturridge dakika ya 33 na 35 na Luis Suarez dakika ya 50.
Ushindi
huo, unaifanya Liverpool itimize pointi 46 baada ya kucheza mechi 23 na
kuendelea kukaa nafasi ya nne, nyuma ya Chelsea pointi 49, Manchester
City pointi 50 na Arsenal pointi 52.

Post a Comment