AZAM YAPANDA KILELENI LIGI KUU, YANGA YABANWA MKWAKWANI
AZAM
FC imepanda kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kufuatia
ushindi wa bao 1-0 jioni hii dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, Uwanja wa
Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Bao pekee la Azam limefungwa na mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche dakika ya 31 kwa shuti kali baada ya kuukuta mpira uliozuiwa na mabeki wa Rhino, kufuatia shuti la ndugu yake kutoka nchi moja, Ismael Kone.
Azam sasa inafikisha pointi 33 na kupanda kileleni, ikiiteremsha Yanga iliyolazimishwa sare ya bila kufungana na Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga leo ambyo sasa inakuwa na pointi 32.

Post a Comment