ad

ad

Yanga yatamba kurudisha heshima Mapinduzi Cup

TIMU ya Yanga SC imeahidi kutoa kipigo kwa timu walizopangiwa, ikiwemo timu ya Tusker ya Kenya wanayotarajia kuanza nayo kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup yaliyopangwa kuanza Januari 2, mwakani Visiwani Zanzibar.

 Yanga inatarajiwa kuondoka jijini Dar Januari Mosi kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mashindano hayo siku ambayo wapinzani wao Simba watashuka dimbani kuvaana na timu ya AFC Leopards ya Kenya.

Akizungumza Kocha Msaidizi wa Yanga, Fredy Minziro, alisema kikosi kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na wanaamini kuwa mazoezi hayo yatawafanya waibuke na ushindi kwenye kila mchezo.

“Tumewaandaa vizuri wachezaji wetu kwa ajili ya mashindano ya Mapinduzi Cup na kurudisha heshima tuliyoipoteza kwenye mchezo wa Nani Mtani Jembe.

 “Kwa sasa wachezaji wako makini wanajituma kwenye mazoezi ili kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mashindano hayo, hawatakiwi kufanya makosa waliyoyafanya kwenye mechi iliyopita,” alisema Minziro.




Powered by Blogger.