Mratibu
wa Tamasha la Ujasiriamali, Abdallah Mrisho (wa pili kulia) akiongea
jambo na waandishi wa habari leo ndani ya ukumbi wa The Atriums Hotel
iliyoko Sinza, Afrika Sana jijini Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha (wa pili kushoto) akiongea
na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni mratibu wa tamasha hilo,
Abdallah Mrisho na kushoto ni H. Baba.
Abdallah Mrisho akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Fid Q naye akielezea namna
atakavyolitumia tamasha hilo kuwajenga vijana wa Mwanza katika maisha
yao kupitia fani yake ya muziki.
Msanii kutoka jijini Mwanza, H. Baba, akielezea namna alivyojipanga kuwafikishia somo la ujasiriamali wakazi wa Mwanza.
Baadhi ya waandishi na wapiga picha (kulia) wakichukua matukio ya habari kuhusu tamasha hilo.
MENEJA Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, ambaye pia ni
mratibu mkuu wa Tamasha la Ujasiriamali linalotarajiwa kufanyika Ijumaa
hii hadi Jumapili jijini Mwanza, Abdallah Mrisho, leo ameongea na baadhi
ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini na kuwaleleza
kuhusu tamasha litakalofanyika siku ya Ijumaa katika Viwanja vya CCM
Kirumba jijini Mwanza ambapo mikakati yote imekamilika.
Mrisho alisema tamasha hilo lililodhaminiwa na Kampuni ya simu za
mkononi ya Tigo, Benki ya NMB na Street University, limeandaliwa
kuwawezesha vijana na wakazi wa Jiji la Mwanza kutambua mbinu
mbalimbali za kujikwamua kimaisha. Watoa mada watakuwa ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Global Publishers Ltd, Eric James Shigongo, James
Mwang’amba, Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji) na Mbunge wa Mbeya
mjini Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’.
Kwa upande wa burudani kutakuwa na wasanii Fid Q, H. Baba, Young
Killer, Jitta Man na Sugu. Pia kutakuwa na wasanii wa muziki wa Injili
ambao ni Martha Mwaipaja atakayeimba sambamba na Masanja Makandamizaji
na Edson Mwasabwite.
(Habari/Picha: Musa Mateja / GPL)
Post a Comment