ad

ad

MUSOTI: OKWI HAKUSTAHILI KUKAA BENCHI YANGA

BEKI makini wa Simba raia wa Kenya, Donald Musoti, amesema kocha wa Yanga, Ernie Brandts, alifanya kosa kumweka mshambuliaji Emmanuel Okwi benchi.
Yanga ilicheza na Simba, Jumamosi iliyopita kwenye mchezo wa kirafiki wa ‘Nani Mtani Jembe’ na kulala kwa mabao 3-1.

Okwi ambaye ndiye alifunga bao pekee la Yanga aliwekwa benchi na kuingia mwanzoni kabisa mwa kipindi cha pili na ndiye aliyeisumbua safu ya ulinzi ya Simba.

Akizungumza  Musoti  alisema Okwi ni mchezaji hatari na anahitaji muda ili aweze kufanya vizuri zaidi kwenye timu yake kwani anamfahamu vizuri na kudai hakupaswa kuanzia benchi.

“Yanga ni timu nzuri, lakini ilikuwa ikicheza kwa kujiamini, walikuwa wakicheza polepole sana, sisi tulikuwa na mbinu yetu ambayo tulikuwa tukiitumia kwa kurudi nyuma kulinda bao letu na kutafuta nafasi jinsi ya kufunga, hali ambayo tulikuwa tukiwachanganya wapinzani wetu.

“Okwi ndiye alikuwa mchezaji pekee aliyecheza katika kiwango kizuri kwa kuwa alivyoingia alijitahidi kuubadili mchezo na kutufanya tushambuliwe na matokeo yake ametufunga.

“Kocha amefanya makosa makubwa sana kwa kumweka benchi kwani naamini angefunga zaidi ya bao moja iwapo kocha angemuanzisha, anaonekana ni mchezaji mzuri sana kwani amekaa muda mfupi tu na timu lakini ameweza kuelewana na wenzake,” alisema  beki huyo.
Powered by Blogger.