ad

ad

YANGA: SIMBA WAMETUBEBA KLABU BINGWA AFRIKA

KLABU ya Yanga imesema kichapo cha mabao 3-1 toka kwa Simba kwenye mchezo wa ‘Nani Mkali Jembe’ kimewafungua macho ya kufanya vizuri kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Uongozi wa timu hiyo umesema ungepata aibu ya mwaka kama wasingecheza mchezo huo dhidi ya Simba kwa kuwa wangejiona wana timu nzuri.

Yanga inatarajiwa kufungua dimba kwenye Michuano ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Komorozine ya Comoro, Februari, mwakani jijini Dar es Salaam.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb, alisema kama wasingecheza na Simba na kupata matokeo kama hayo basi wangeathirika zaidi kwenye michuano ya kimataifa.

Alisema wamewapa changamoto kubwa na mikakati mipya ya kukiunda kikosi chao kwa kuwa tayari wameshajua upungufu wao mapema.

“Ni vyema tulivyoona upungufu wetu kupitia mechi yetu ya kirafiki na Simba vinginevyo si ajabu ingekuwa aibu sana kwenye Michuano ya Klabu Bingwa tunayotarajia kushiriki.
“Yaani tungeathirika zaidi lakini sasa tumejijua tupo kwenye hali gani,” alisema Bin Kleb.
Kama wakifanikiwa kuitoa timu hiyo ya Comoro Yanga itavaana na Al Ahly ya nchini Misri kwenye hatua itakayofuata

Powered by Blogger.