YANGA YAKAA KIKAO NA KASEJA KWA SAA TATU
BAADA ya kutua Yanga KOCHA wa makipa wa Yanga,
Razack Siwa, amesema alitumia zaidi ya saa tatu kumweka sawa
kisaikolojia kipa Juma Kaseja siku moja baada ya mechi dhidi ya Simba.
Akizungumza Siwa, raia wa Kenya, alisema baada ya mechi hiyo kumalizika siku iliyofuata alimuita
Juma na kukaa naye kujadili hasa kuhusiana na bao la tatu ambalo lililalamikiwa na kila mtu.
“Nilikaa na Juma baada ya mechi kwa saa tatu nikamwambia ni sehemu ya mchezo na anatakiwa kuwa sawa lakini pia kama kocha niliumizwa sana na lile bao la tatu alilofungwa na sasa namfanyisha mazoezi ya mtindo kama wa bao hilo tulilofungwa,” alisema Siwa.
Kaseja alifungwa bao hilo baada ya kugeuka na mpira aliokuwa amepasiwa langoni mwake na ndipo kiungo mshambuliaji wa Simba, Awadhi Juma, alipounasa na kufunga bao safi kwenye mchezo huo wa kirafiki maarufu kama ‘Nani Mtani Jembe’.
Kipa mpya wa Yanga, Juma Kaseja.
Kaseja alitupiwa lawama kibao kutoka kwa mashabiki na wanachama wa
klabu hiyo kutokana na kuruhusu bao jepesi kwenye mechi dhidi ya watani
wao, Simba, Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam na matokeo kumalizika kwa Simba kushinda 3-1.Akizungumza Siwa, raia wa Kenya, alisema baada ya mechi hiyo kumalizika siku iliyofuata alimuita

Post a Comment