MASHAUZI CLASSIC YATIMIZA MIAKA MITATU
Keki iliyoandaliwa kwa ajili ya
sherehe hiyo ya kutimiza miaka mitatu.
Ndugu pamoja na marafiki wa Isha
wakikata keki kwa pamoja.
Wanenguaji hao wakifanya yao
jukwaani kama wanavyoonekana.
BENDI ya muziki wa taarabu Mashauzi
Classic inayoongozwa na mwanadada Aisha Ramadhani Makongo 'Isha Mashauzi' usiku
wa kuamkia leo (Ijumaa) imetimiza miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza na mtandao huu
mkurugenzi mtendaji wa bendi hiyo Isha Mashauzi alisema kuwa anamshukuru Mungu
kwa kumfikisha miaka mitatu tangu kuanzisha bendi yake hiyo.
"Kiukweli napenda kuchukuwa
fursa hii kumshukuru Mungu, mama yangu mzazi mdogo wangu Saida Ramadhani
'Sungura mjanja' kwa kuwa pamoja kulisukuma gurudumu hili la kuisimamia bendi
ya Mashauzi kikamilifu hadi leo kufikia hatua ya kutimiza miaka mitatu"
alisema Isha.
Post a Comment