TAMASHA LA KRISMASI LAFANA UWANJA WA JAMHURI, MOROGORO
Mwimbaji
Edson Mwasabwite akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki wake wakati
akitumbuiza kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro jana jioni.
Boniface Mwaitege naye akawanyanyua kwenye viti mashabiki waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo.
Mwanamama mwenye sauti ya mirindimo Upendo Nkone akikonga nyoyo za mashabiki wake.
Mwimbaji
wa muziki wa injili Rose Muhando akiimba katika tamasha la Krismasi
lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro
likishirikisha waimbaji mbalimbali wa muziki huo hapa nchini na mwimbaji
wa kimataifa kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti ambao kwa ujumla
walisuuza mioyo ya mashabiki baada ya kushusha burudani ya nguvu katika
tamasha hilo. Tamasha hilo liliandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya
jijini D es Salaam. (PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE-MOROGORO)
Mwanamama mwingine Upendo Kirahiro akiwaimbisha mashabiki wake.
Hapa akiimba kwa furaha kumtukuza Mungu wake mbele ya mashabiki kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Vijana wa kazi kutoka kundi la Kitimtim la Rose Muhando wakionyesha umahiri wao katika kucheza.
Mwimbaji Edson Mwasabwite akiimba na mmoja wa mashabiki wake katika tamasha hilo.
Mwimbaji wa kimataifa kutoka Zambia, Ephraim Sekereti, akiimba jukwaani katika tamasha hilo.
Hapa akiimba na mashabiki wake.
Upendo Nkone akicheza na vijana wake.

Post a Comment