ARSENAL YASHIKWA YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA EVERTON
Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la kuongoza katika dakika ya 80 ya mchezo.
Timu ya Arsenal imeshikwa baada ya kutoka sare ya 1-1 na Everton
katika mechi ya Ligi Kuu England iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini
London, Uingereza hivi punde.
Bao la kuongoza la Arsenal limewekwa kimiani na Mesut Ozil dakika ya
80 kabla ya Gerard Deulofeu kusawazisha bao hilo dakika ya 84 na kufanya
matokeo kuwa 1-1.
Mpaka mwisho wa mchezo Arsenal 1 na Everton 1. Kwa matokeo hayo bado
Arsenal wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 35 wakati Everton wapo
nafasi ya tano wakiwa na pointi 28.

Post a Comment