NIYONZIMA ANG’ARA TUZO ZA MWANASPOTI 2013
![]() |
| Haruna na tuzo zake tatu |
Na Mahmoud Zubeiry, Mlimani City
KIUNGO wa Yanga SC, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima raia wa Rwanda, ameshinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa gazeti la Mwanaspoti, akiwashinda Amri Kiemba, Shomary Kapombe wa Simba SC na Themi Felix wa Kagera Sugar.

Katika
hafla iliyofana kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam na
kuhudhuriwa na wachezaji wengi, mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri wa
(TEKNOHAMA) Januari Makamba, mchezaji Niyonzima aliondoka na tuzo tatu,
nyingine ya mchezaji wa kigeni na 11 Bora wa Mwanaspti.
![]() |
| Haruna akipokea tuzo yake ya Mwanasoka Bora wa Kigeni kutoka kwa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA) |
Katika tuzo ya mchezaji bora wa kigeni, Niyonzima aliwashinda mchezaji mwenzake wa Yanga, mshambuliaji wa Kiganda, Hamisi Friday Kiiza na mshambuliaji wa Azam kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche.
Mchezaji
wa Azam FC, Joseph Kimwaga aliwashinda Juma Luizio wa Mtibwa Sugar na
Ramadhani Singano ‘Messi’ katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mchezaji
Chipukizi.
Mwanahamisi
Omar wa Mburahati Queens aliwashinda Shelida Boniface na Fatuma Mussa
katika ya Mchezaji Bora wa kike, wakati Mbwana Samatta aliwashinda Henry
Joseph aliyekuwa anacheza Kongsvinger ya Norway kabla ya kurejea Simba
SC msimu huu na mshambuliaji mwenzake wa TP Mazembe ya DRC, Thomas
Ulimwengu katika tuzo ya mwanasoka anayecheza nje.
Oden Mbaga aliwashinda Martin Sanya na Ibrahim Kidiwa katika tuzo ya Refa bora, wakati Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ aliwashinda Muingereza Stewart Hall wa Azam na Mholanzi Ernie Brandts wa Yanga katika tuzo ya kocha bora.

Thomas
Ulimwengu alishinda tuzo ya bao bora alilofunga katika mechi dhidi ya
Ivory Coast kuwania tiketi ya Kombe la Dunia, wakati Kipre Tchetche
ameshinda tuzo ya Mfungaji bora.
Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, David Mwantika, Amri
Juma Kaseja, Mbuyu Twite, Shomary Kapombe, Kevin Yondan, David Mwantika, Amri
Kiemba, Thomas Ulimwengu, Haruna Niyonzima, Themi Felix, Mbwana
Samatta na Kipre Tchetche wameteuliwa katika ’11 Bora’ wa Mwanaspoti.
Zilizotolewa
pia tuzo za heshima kwa wachezaji wa zamani nchini akina Nicholas
Akwitende, John Lyimo, Mbwana Abushiri, Omar Zimbwe, Jellah Mtagwa na
mtangazaji wa zamani maarufu, Mshindo Mkeyenge.
Mkeyenge
aliyeanza kutangza tangu miaka ya 1960 Radio Tanzania (RTD)
aliwahuzunisha wengi baada ya kuwasili jukwaani akiwa amebebwa kutokana
na kukatwa mguu kwa sababu ya maradhi ya kupooza.
Hadhara
Charles alipewa tuzo ya kipaji maalum, wakati Rais wa Baraza la Vyama
vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Leodegar Tenga alipewa tuzo
ya Utawala Bora katika soka. Washindi walipewa na zawadi za fedha,
Niyonzima Sh. Milioni 5, wengine Sh. Milioni 1 na wengine 500,000.
Kwa ujumla tuzo hizo zilizosindikizwa na burudani ya wanamuziki Juma Nature, Joh Makini na King Kiki zilifana.
CHANZO CHA HABARI NA BINZUBEIRY BLOG

Post a Comment