Nani kamkosea Chidi Benz? Tweet zake zaacha utata
Hakuna tena kitu kizuri kwa Chidi Benz siku hizi. Kwa muda
mrefu rapper huyo ambaye hivi karibuni ametokea kukubalika sana nchini
Kenya (thanks kwa mashavu anayopewa na Nonini) ameonekana kutoa yake ya
rohoni yanayomuumiza kupitia Twitter.
Yeye na Wakazi kuna tatizo?
Picha lilianza , baada ya Wakazi kutweet: Na ningependa kusema
pia AY, Dimpoz, Ally Kiba, FidQ, Shaa, Cpwaa, Black Rhino, Remi Ongala,
Profesa Jay & Lady Jaydee ni other Local heros!
Baada ya kuona ujumbe huo wa Wakazi, Chidi alimuuliza kishari ‘nini?’
Wakazi alichuna. Chidi akaamua kuandika: Hujui kuongea huwezi
muoga..unaweza kuandika hapa twitter. Nyie ndio mkianza kushindwa
mnasifia maadui.#umal** tuu.”
Ujumbe huo ulivuta hisia za watu wengi akiwemo Madee aliyeuliza:
Rasheeed nani tena kazingua? Chidi alijibu: Mazafanta wanahisi wanajua
kuliko wewe wakati mwenyewe saa zingine unaona hujijui..2
Hata hivyo hatuwezi kuthibitisha kama maneno hayo yalikuwa yakimlenga
Wakazi ama mtu mwingine kwakuwa kabla ya hapo tayari alikuwa ameanza
kuandika tweets za hasira.
“Game ilipo now na propaganda zake inaua vitu vingi tu.sisi
tunaonekana tunalalamika ujinga but hatuna maisha mabaya. Viongozi wa
nchi sio lazima mdil na bongo freva..haiongezi wewe kufatwa but
unatuongezea uadui usio na lazima. Mi natangazwa kwa ubaya tuuuuu.ila
nina marafiki bado na wengi wanaongezeka hata hapa.#nakaza roho,”
aliandila Chidi.
Kunani?

Post a Comment