ad

ad

Global FC kuwavaa Bagamoyo Veterani kesho

Na Shafii Hashim
BAADA
ya wikiendi iliyopita timu ya Global Publishers FC kuibuka na ushindi wa kibabe wa bao 1-0 dhidi ya Chuo cha Dar es Salaam City (Dacico), kesho Jumamosi timu hiyo inatarajiwa kuelekeza nguvu zake kwenye mechi yao kabambe dhidi ya Bagamoyo Veterani.
Mechi hiyo itakayopigwa Bagamoyo, Pwani, ni moja kati ya ziara nyingi za mikoani za kimichezo za timu hiyo zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili kukiweka sawa kikosi kwa ajili ya michuano mingi ya kuufunga mwaka 2013 na kuukaribisha 2014.

Nahodha wa timu hiyo yenye maskani yake maeneo ya Mwenge jijini Dar, Phillip Nkini ameliambia gazeti hili kuwa, mara baada ya mechi ya Bagamoyo, ziara yao hiyo itaendelea kwenye mikoa ya Tanga, Morogoro na visiwani Zanzibar.

Alisema wakiwa huko, wachezaji wa Global ambao pia ni waandishi wa Gazeti la Championi, watapata fursa ya kuzungumza na wasomaji wao kujua wanahitaji nini zaidi kwenye magazeti ya Championi ili wazidi kulifurahia zaidi gazeti hilo bora la michezo Tanzania.

“Baada ya mechi ya Bagamoyo, tutaelekea Tanga, Morogoro na Zanzibar kwa ajili ya kwenda kukipiga huko na kuzungumza na wasomaji wetu,” alisema Nkini.
CREDIT: GPL
Powered by Blogger.