ad

ad

MISS ARUSHA AOLEWA NA MJESHI MMAREKANI

MISS Arusha na Tanzania namba 3 mwaka 2001, Sharon Pownall amefunga ndoa na mwanajeshi wa jeshi la majini la Marekani aliyefahamika kwa jina moja la Dylan.
Tukio hilo lililogusa hisia za watu wengi lilitokea hivi karibuni mjini hapa, lilifanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Ngurudoto na kuhudhuriwa na mamia ya watu.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichohudhuria harusi hiyo iliyofungwa kanisani, kulikuwa na kikundi cha watu ambacho hakikupenda kuona miss huyo akiolewa kiliisengenya ndoa hiyo.
“Kuna kikundi cha watu kilikuwa hakipendi kuona Sharon anaolewa hivyo kilikuwa kikipambana chinichini kuhakikisha ndoa hiyo haifungwi lakini bahati mbaya kimeshindwa,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo, pamoja na kampeni hizo za kuvuruga ndoa hiyo, kwa upande wake Sharon alimshukuru Mungu kwa kufanikisha ndoa hiyo aliyokuwa akiisubiri kwa hamu.
“Namshukuru Mungu kwa kuwa kila kitu kimekwenda vizuri na sasa nimekuwa mke kamili wa ndoa, kama kuna mtu alikuwa na kijiba cha roho atabaki nacho milele,” alisema miss huyo.
Powered by Blogger.