KOCHA MPYA AZAM FC ATUA, ATAMBULISHWA RASMI
KOCHA mpya
wa Azam FC Joseph Omog hatimaye leo ametua rasmi jijini Dar tayari kwa kuanza
kazi ya kukinoa kikosi hicho.
Omog raia wa
Cameroon ametua leo saa 3:00 asubuhi na Ndege ya Shirika la Kenya ambapo mara
baada ya kuwasili alipelekwa moja kwa moja katika ofisi kuu za timu hiyo
zilizopo Mzizima na kusaini mkataba wa miaka miwili.
Mara baada
ya kusaini mkataba huo Omog anayechukua nafasi ya Muingereza Stewart Hall
alitambulishwa rasmi kwa waandishi wa habari na mwenyekiti wa timu hiyo Said
Mohamed ambaye alimtaja kocha huyo kuwa ni kati ya makocha bora sita
wanaopatikana Bara la Afrika.
Mohamed
maarufu kama Mzee Said amesema Azam inafuraha kubwa kumpata Omog ambaye uongozi
wa timu hiyo umeona ndiye anayestahili kuchukua nafasi ya Stewart aliyesitisha
mkataba mwezi uliopita.
Omog kwa
upande wake kocha wa zamani wa kikosi cha A.C Leopards ya Congo Brazaville
alionyesha kushangazwa na mapokezi aliyoyapata ambapo amesema mara baad ya
kusaini mkataba huo sasa kazi yake kubwa ni kuhakikisha timu hiyo inaoata
mafanikio ndani ya uwanja
Kivutio
kikubwa katika ujio wa kocha huyo ni kuja na mwanaye Henry Omog ambaye ni beki
wa zamani wa Canon de Yaunde huku akiwa
ndiye meneja wa baba yake huyo.
Post a Comment