BERKO ATUA SIMBA, AHAHIDI KUPAMBANA NA DHAIRA
ALIYEKUWA
kipa wa Yanga Mghana Yaw Berko ametua leo jijini Dar tayari ya kuanza maisha
mpya na Simba SC.
Berko ametua jijini leo asubuhi na ndege ya
Shirika la Kenya akitokea kwao Ghana na kulakiwa na kiongozi wa ufundi wa Simba
Danny Manembe.
Mara baad ya
kutua Berko alipata nafasi ya kuzungumza na Salehjembe akisema anaijua Simba
vizuri huku pia akimjua kipa wao namba moja Abel Dhaira ambapo atahakikisha
anapambana katika mazoezi ili kujihakikishia nafasi katika timu hiyo.
“Naijua
Simba, mimi sio mgeni hapa, namjua pia kipa wao yule wa Uganda lakini
namtanguliza Mungu, lakini pia nitajituma mazoezini ili kuweza kujipatia
nafasi.

Post a Comment