KINANA AMALIZA ZIARA YAKE KATIKA JIMBO LA TUNDURU KUSINI, KESHO NI TUNDURU KASKAZINI
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kulia akiwa na
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr. AshaRose Migiro na
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi ,wakishiriki katika
ujenzi wa daraja la Lukumbo Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wakati akiwa
katika ziara yake ya kikazi yenye lengo la kukagua ilani ya uchaguzi wa
Chama cha Mapinduzi na kukagua miradi ya maendeleo huku akihimiza
wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo ili kujiletea maendeleo
huku Serikali ikipanga mipango ya maendeleo na kuleta chachu ya
maendeleo nchini, Katibu Mkuu huyo pamoja na ujumbe wake kesho
wanaendelea na ziara yao katika jimbo la Tunduru Kaskazini baada ya
kumaliza ziara katika jimbo la Tunduru Kaskazini linaloongozwa na Mh.
Mtutura Abdallah Mtutura.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katikati akiongoza wananchi kwa
kukimbia mchakamchaka kuelekea shule ya sekondari ya kata ya Mchoteka
ambako alishiriki katika shughuli za ujenzi wakati aliposhiriki kuchimba
msingi wa maabara ya shule hiyo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr. AshaRose Migiro katikati na
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi wakishiriki katika
ujenzi wa daraja la Lukumbo wilayani Tunduru.
Wazee wa kijiji cha Lukumdo wakimsubiri mgenzi rasmi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Oddo Munisi Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma wakikagua daraja la Kukundo
Mkazi wa kijiji cha Lukunbo Bi. Mwanabibi Kasembe akielezea furaha yake mara baada ya kuanza kwa ujenzi wa daraja hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiuliza jambo wakati alipokagua ujenzi wa daraja hilo leo.
Wanahabari wakiwajibika katika ziara hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Tunduru Kusini Mh. Mtutura Abdallah Mtutura akizungumza
wakati Ndugu Abdulrahman Kinana alipokagua ujenzi wa nyumba za walimu
katika shule ya sekondari ya kata ya Mchoteka leo Kulia ni Nape Nnauye
na kutoka kushoto ni Dr. Asha Rose Migiro huku Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana akisikiliza.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi katika kata ya
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na viongozi wengine wakishiriki
katika uchimbaji wa msingi wa maabara ya shule ya sekondari ya Mchoteka
Wilayani Tunduru leo.
Akina mama wakicheza ngoma ya asili katika uwanja wa mkutano kwenye kata ya Mtina Wilayani Tunduru
Katibu
wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr. AshaRose Migiro akisalimia
wananchi katika mkutano wa hadhara kwenye kata ya Mtina Wilayani
Tunduru.
Kikundi cha Ngoma kikitumbuiza katika kata ya Mtina leo
Mkuu
wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwasilimia wananchi wa Kata ya Mtina
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mtina.
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi akizungumza na wana
Mtina kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo leo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiwahutubia wananchi wa kata ya Mtina katika wilaya ya Tunduru.
(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-TUNDURU
KUSINI)
Post a Comment