FUMANIZI LA JB UTATA MTUPU
STAA wa
filamu Bongo, Jacob Steven ‘JB’ hivi karibuni amedaiwa kufumaniwa hotelini na mke wa mtu
wakivunja amri ya sita.
Jacob Steven ‘JB’
Tukio hilo
lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli ya Royal Village iliyopo Dodoma
ambapo JB alikutwa na mke wa mtu aliyetambulika kwa jina la Sara wakivunja amri
ya sita.
ISHU ILIKUWA
HIVI
Akizungumza
kwa masikitiko mume wa Sara ambaye ni dj maarufu Dodoma, Dj Rama alisema
alifuatilia nyendo za mkewe huyo kwa siku nzima na mawasiliano yake ambapo ambapo
kwa muda mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambaye waliagana kukutana katika
hoteli hiyo.
Ilipofika
saa tatu usiku Dj Rama alifika ndani ya hoteli hiyo na kuingia na kwenda
kugonga kwenye chumba alichokuwa amelala na mwanamke huyo ambapo aligonga kwa
muda mrefu baadaye sana ndipo mlango ukafunguliwa.
JB ASHUSHIWA
KIPIGO
Baada ya
mlango kufunguliwa JB alipokea kipigo
cha haja kutoka kwa dj huyo ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa
wanafanya doria katika shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa
hoteli hiyo walienda kumuokoa huku
mwanamke aliyekuwa naye akitoroshwa kimyakimya.
Baada ya
kuokolewa JB na mume wa mtu huyo walipelekwa katika kituo cha polisi cha Area D
ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa kesho yake warudi.
Dj Rama
aliendelea kueleza kuwa kesho yake waliporudi polisi alishinikizwa kuwa akubali
yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
WALIKUTANAJE
NA JB?
Kwa mujibu
wa mume alisema alipojaribu kumuuliza mkewe huyo walikutana vipi na JB
alimweleza kuwa walikutana club ambapo walibadilishana namba na kuendelea
kuwasiliana.
Mwanamke
huyo aliyeshikwa ugoni hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka leo ambapo
mumewe alieleza kuwa amuhitaji tena kwani alikuwa mchumba wake bado hawajafunga
ndoa.
“Mimi
simuhitaji tena japokuwa ana mimba ya miezi mine na sina uhakika kama ni ya
kwangu kwani tabia zake sizielewi kabisa bora niachane naye naamini Mungu atanipatia mwanamke sahii
kwangu,”alisema Dj Rama.
JB ALIFUATA
NINI DODOMA?
Dj Rama
alieleza kuwa JB alienda Dodoma kwa mwaliko wa wasanii wa filamu waliokuwa
wanazindua filamu yao na kumfanya yeye kuwa mgeni rasmi ndipo akapata nafasi ya
kufanya ufuska huo.
JB
ANASEMAJE?
Mapaparazi
wetu walimtafuta kwa hali na mali JB kwa njia ya simu lakini baada ya mwandishi
kujitambulisha na kabla hajazungumza chochote JB alisema amuache kwanza kwani
yupo bize na shooting.
Habari na Mapaparazi
wetu.

Post a Comment