ZITTO KABWE: SERIKALI KIKWAZO UTOROSHAJI WA FEDHA.
Wakati shinikizo
la Dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na Utoroshaji
wa fedha kutoka nchi za Kiafrika, serikali ya Tanzania inavuta miguu.
Moja ya njia ya Serikali za nchi maskini kupata taarifa za makampuni
makubwa ya kimataifa(MNCs) yanayokwepa kodi ni mfumo wa kupashana
taarifa (automatic exchange of tax information) .
Kufutia shinikizo
la nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa "secrecy jurisdictions"
(tax havens) Zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa taarifa.
Tanzania mpaka sasa haijaweka sahihi na serikali haijatoa taarifa yeyote
kwa Umma.
Ghana,
Afrika Kusini na Nigeria nchi zinazotegemea sana rasilimali kama
Tanzania zimeweka saini mkataba huu tayari. Asilimia 44 ya fedha za
kigeni nchini zinatokana na mauzo ya madini nje. Makampuni ya madini
ndio yanaongoza kukwepa kodi.
Tanzania inapoteza jumla ya dola za
kimarekani kati ya milioni 500 na bilioni 1.25 kwa mwaka kutokana na
Makampuni makubwa ya kimataifa kukwepa kodi. Hii ni sawa na kusema
Tanzania inapoteza dola takribani milioni mbili kila siku kwa uporaji
huu.
Naitaka serikali kutoa taarifa kwa nini haichuki hatua kuzuia
mwanya huu wa mapato ya Umma. Serikali ichukue hatua mara moja
kuhakikisha Tanzania inaingia makubaliano ya kupashana taarifa za
kikodi. Huu sio wakati wa kuvuta miguu katika suala nyeti la umma.
Badala ya kukimbilia kutoza kodi wanyonge, tuhakikishe makampuni makubwa
yanayonyonya rasilimali zetu yanalipa kodi inayotakiwa.
Zitto Kabwe, MB
Waziri Kivuli wa Fedha
24 Oktoba, 2013
Geneva, Switzerland
Zitto Kabwe, MB
Waziri Kivuli wa Fedha
24 Oktoba, 2013
Geneva, Switzerland

Post a Comment