MWANAMKE AKAMATWA KWA UJAMBAZI ARUSHA
Arusha
Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi baada ya kufanya jaribio la kuiba simu na fedha katika duka moja maeneo ya Shamsi jijini hapa.
Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi baada ya kufanya jaribio la kuiba simu na fedha katika duka moja maeneo ya Shamsi jijini hapa.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, ACP Liberatus Sabas amesema hivi
karibuni kuwa mwanamke huyo alikamatwa baada ya kuingia katika duka
moja akiwa na mwanaume mmoja jambazi na kumtishia muuzaji ili awape
fedha za M-Pesa na simu zilizokuwepo dukani humo huku akiwa na bastola
mkononi.
“Kulikuwa na mteja mmoja jirani ambaye alimpiga kichwa mwanamke huyo
na akaanguka chini, purukushani ikaanza na yule mwanaume aliyekuwa naye
akakimbia na kwa kuwa kulikuwa na askari doria walikuwa wanapita eneo
hilo, walimkamata mwanamke huyo,” alisema kamanda Sabas.
Akifafanua zaidi, kamanda huyo alisema alipofikishwa kituo kikuu cha
polisi alihojiwa na kuwataja wenzake wanne ambao baada ya msako
walikamatwa na walipopekuliwa nyumbani kwao walikutwa na shotgun moja,
risasi, simu ya upepo pamoja na sare ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania na
buti zake.

Post a Comment