MATUKIO MKOA WA MBEYA
WILAYA YA CHUNYA – KUPATIKANA NA SARE ZA ASKARI WANYAMA PORI NA PINGU.
Mnamo tarehe 18.10.2013 majira ya saa 7:00 mchana, katika kijiji cha
Bitimanyanga, kata ya Mafyeko, tarafa ya Kipembawe wilaya ya Chunya
mkoa wa Mbeya. Askari polisi wakiwa doria/msako kwa kushirikiana na
askari wanyamapori walimkamata Samwel s/o Vitalis @ Mande , miaka 34,
Mnyaturu, mkulima, mkazi wa kijiji cha Bitimanyanga akiwa na sare pair
moja “kombati” za askari wa wanyamapori pamoja na pingu moja. Mbinu ni
kutumia vifaa hivyo katika uwindaji haramu.
Taratibu za kisheria zinafanywa ili afikishwe mahakamani. Kamanda wa
polisi mkoa wa Mbeya kamishna msaidizi wa polisi Diwani Athumani anatoa
wito kwa jamii kuacha kumiliki mali za serikali isivyo halali kwani ni
kosa la jinai. Aidha anaendelea kutoa rai kwa yeyote mwenye taarifa juu
ya mtu/watu au kikundi kinachomiliki mali za serikali /wawindaji
haramu azitoe katika mamlaka husika ili wahusika wakamatwe na sheria
ichukue mkondo wake.
WILAYA YA MBEYA MJINI – KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI(GONGO).
Mnamo tarehe 21.10.2013 majira ya saa 6:00 mchana, katika mtaa wa
Manga –Mwanjelwa , kata ya Manga , tarafa ya Iyunga jiji na Mkoa wa
Mbeya. Askari polisi wakiwa doria/msako waliwakamata
- Itika d/o kimanga,, 41, kyusa, mkulima, mkazi wa mwanjelwa
- Yasiwa s/o shelisheli,miaka 37, mnyiha, kulima, mkazi wa manga,
- Mateso s/o shelisheli,miaka 33, mnyiha,mkulima, mkazi wa chunya na
- Emanuel s/o silavwe,miaka 33, mnyamwanga, kulima, mkazi wa manga wakiwa na pombe haramuya moshi (gongo) ujazo wa lita nane (08).
Watuhumiwa ni wauzaji nawatumiaji wa pombe hiyo. Taratibu za
kisheria zinafanywa ili wafikishwemahakamani. Kamanda wa polisi mkoa wa
mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani athumani anatoa wito kwa
jamii kuacha kutumia pombe haramu ya moshi (gongo) kwani ni kinyume cha
sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
WILAYA YA MOMBA – KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe 21.10.2013
majira ya saa 11:00 alfajili, katika mtaa wa Mjini, kata ya Tunduma ,
tarafa ya Tunduma wilaya ya Momba mkoa wa Mbeya. Askari polisi wakiwa
doria/msako walimkamata
- Edmund s/o kanfwa, miaka 41, kyusa, mkulima, mkazi wa mwanjelwa na
- Taifa s/o Mwamahonje, miaka 22, Mmalila, Mkulima wote wakazi wa Migombani – Tunduma wakiwa na bhangi kete 18 sawa na uzito wa gram 90.
Watuhumiwa ni wauzaji na wavutaji wa bhangi. Taratibu za kisheria zinafanywa ili wafikishwe mahakamani.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishna msaidizi wa polisi diwani
athumani anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia dawa za kulevya kwani ni
kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
(IMETOLEWA NA DIWANI ATHUMANI - ACP) KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Post a Comment