MAN UNITED YAPAA KILELENI KUNDI A
BAO
la kujifunga la Inigo Martinez mapema dakika ya pili limetosha kuipa
Manchester United ushindi wa 1-0 dhidi ya Real Sociedad Uwanja wa Old
Trafford usiku huu na kupanda kileleni mwa Kundi A katika Ligi ya
Mabingwa Ulaya.
Martinez
alijibabatiza mpira na kuudondoshea kwenye nyavu za timu yake sekunde
ya 69 katika jitihada za kuokoa mpira uliopigwa Wayne Rooney.
United inapanda kileleni baada ya Shakhtar kufungwa 4-0 na Bayer Leverkusen ikitimiza pointi saba baada ya mechi tatu.
Man Utd: De Gea, Rafael/Smalling dk59, Jones, Evans, Evra,
Valencia, Carrick, Giggs, Kagawa, Hernandez/Young dk80 na Rooney.
Real
Sociedad: Bravo, Carlos Martinez, Mikel Gonzalez, Martinez, De la
Bella, Vela, Zurutuza/Castro dk75, Markel, Prieto/Pardo dk68, Griezmann
na Seferovic/Agirretxe dk75.
Katika
mechi nyingine zilizochezwa usiku huu, CSKA Moskva imelala 2-1 mbele ya
Manchester City. Mabao ya City yalifungwa na Sergio Aguero dakika za 34
na 42, yote pasi za Negredo, wakati bao la wenyeji lilifungwa na Tosic
dakika ya 32, pasi ya Honda.
Mabao
mawili ya Cristiano Ronaldo dakika ya nne na 29 yameipa Real Madrid
ushindi wa 2 - 1 dhidi ya Juventus, ambayo bao lake lilifungwa na
Llorente dakika ya 22.
Galatasaray
imeifumua mabao 3 - 1 Kobenhavn, mabao yake yakifungwa na Felipe Melo
dakika ya 10, Wesley Sneijder dakika ya 38 na Didier Drogba dakika ya
45, wakati bao pekee la wapinzani wao limefungwa na Claudemir dakika ya
88.
Anderlecht
imefungwa nyumbani 5-0 na PSG, Zlatan Ibrahimovic akifunga mabao manne
dakika za 17, 22, 36 na 62, lingine likifungwa na Cavani dakikya 51,
wakati Benfica imelazimishwa sare ya 1 - 1 nyumbani na Olympiakos
Piraeus.
Mabingwa
watetezi, Bayern Munich wameendeleza umwamba, baada ya kuifumua
Viktoria Plzen 5-0, mabao ya Ribery dakika ya 25 na 61, Alaba dakika ya
37, Schweinsteiger dakika ya 64 na Gotze dakika ya 90. 
Mistake: Inigo Martinez's early own goal gave Manchester United a perfect start at Old Trafford
Rebound: Wayne Rooney's original shot hit the post before Martinez put the rebound into his own net
Joy: Javier Hernandez, Ryan Giggs and Rooney celebrate the opening goal
Ruled out: Hernandez had a goal disallowed for offside during the first half
Pensive: Manchester United manager David Moyes shouts some instructions from the sidelines
Familiar face: Former United boss Sir Alex Ferguson was in the stands at Old Trafford

Post a Comment