RAIS BARACK OBAMA AWASILI TANZANIA
Rais wa Marekani Barack Obama, amewasili nchini Tanzania katika mkondo wake wa mwisho wa ziara yake barani Afrika.
Ziara ya Obama inasemekana kulenga kuimarisha
uhusiano wa kibiashara na Afrika huku kukiwa na wasiwasi kuwa Marekani
inaachwa nyuma na China katika uhusiano wao na Afrika.

Obama amewasili Tanzania baada ya ziara yake ya Afrika Kusini ambako rais mstaafu Nelson Mandela anaugua.
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na familia yake
pamoja na maafisa wake wa serikali na wacheza densi za kitamaduni
walimkaribisha Obama na familia yake mjini Dar es Salaam.
Baadhi ya wananchi wa Tanzania kupitia mitandao
ya kijamii wamekosoa ziara ya Obama katika nchi yao, wakisema kuwa ziara
yake imeathiri shughuli za maisha yao ya kila siku.
Obama alitembelea Senegal kabla ya kupitia
Afrika Kusini na kisha Tanzania ambako ziara yake ya Afrika inaishia
kabla ya kurejea Marekani.
PICHA ZA MATUKIO KUWAJIA BDAE
PICHA ZA MATUKIO KUWAJIA BDAE
Post a Comment