KUTANA NA SARAKASI ZA PREZZO KWA WAREMBO.
JACKSON Ngechu Makini ‘CMB Prezzo’ alizaliwa siku ya Jumatano ya Januari
09, mwaka 1980. Ni rapa lejendari wa Kenya ambaye alikuwa mmoja wa
mastaa waliowakilisha nchi zao katika Shindano ya Big Brother Africa
‘StarGame’, 2012.
Kama ulikuwa hujui, jamaa alizaliwa katika Jiji la Nairobi miaka 33
iliyopita, alikulia maisha ya kitaani eneo la Eastleigh na atakuwa mmoja
wa wanamuziki wakali watakaoshusha bonge la burudani katika Tamasha la
Matumani 2013 litakolofunga mitaa ya Jiji la Dar na viunga vyake kwenye
Uwanja wa Taifa, Julai 7, mwaka huu.
Prezzo ni mwanamuziki mkubwa
ambaye alianza ‘kuhaso’ katika muziki miaka mingi, alikuja kuwika kwenye
miaka ya mwanzoni mwa karne ya 21.
Pamoja na kukumbana na
vipingamizi vingi, nyota ilikuja kung’aa baada ya nyimbo zake kukubalika
kwa maelfu ya mashabiki wake waliokuwa wakizisikiliza, kuziomba kwenye
stesheni mbalimbali za redio na runinga huku wakihudhuria katika
matamasha yake ya wazi na klabu.
Albam
yake ya kwanza ni Naleta Action aliyoiachia mwaka 2004 ikiwa na ngoma
zilizoshika kama Naleta Action, Lets Get Down, Mahangaiko, Leo ni Leo,
Mimi na Wewe, Mafans na nyingine zilizobamba.
Katika albam hiyo, jamaa alimshirikisha mama yake ambaye aliimba mistari kadhaa katika moja ya nyimbo zake.
Albam
hiyo iliuza nakala nyingi na kumfanya Prezzo kuamini kuwa alishakubali
Afrika Mashariki kutokana na aina ya ngoma zake zenye hisia.
Prezzo anajulikana kutokana na aina ya maisha ya gharama anayopendelea kama kuvaa mikufu ya bei ghali, nguo, magari ya vitu vingine vya kitajiri.
Prezzo anajulikana kutokana na aina ya maisha ya gharama anayopendelea kama kuvaa mikufu ya bei ghali, nguo, magari ya vitu vingine vya kitajiri.
Baadaye
mtu mzima Prezzo alishirikishwa kwenye ngoma ya Tazama Mbele ya
aliyewahi kuwa mpenzi wake wa kipindi hicho iliyotengenezwa na Ennovator
wa Samawati Productions huku video yake ikisimamiwa na Ted Josiah.
Ngoma hiyo ilifanya vizuri kwa kushika namba moja kwa wiki nane katika
stesheni mbalimbali za redio na runinga Afrika Mashariki.
Mwaka 2006,
Prezzo aliachia singo mpya ya P.R.E.Z.Z.O ambapo video yake ilisimamiwa
na Ted Josiah wa Blu Zebra. Video ilikuwa kali lakini ilikutana na
maneno mengi ikidaiwa ilitengenezwa kwa gharama kubwa sana ya Sh.
500,000 za Kenya. Hakukuwa na video iliyokuwa imetumia kiasi hicho cha
fedha kwa wakati huo.
Ulipita ukimya kidogo, akiendelea kugonga shoo
za ndani na nje ya Afrika Mashariki, Nigeria na Ulaya. Baadaye
aliendelea na mtindo wa kuachia singo mojamoja kama Liqher, My City My
Town, Unataka Nini, 4sho 4shizzy aliyomshirikisha Ulopa, Nipe Nikupe
aliofanya na AY na Celebration of Life aliyoachia hivi karibuni
akimshirikisha Chess.
BIG BROTHER AFRICA ‘STARGAME’ 2012
Prezzo aliingia kwenye kinyang’anyiro cha BBA ‘StarGame’ 2012 baada ya kuona ni kitu kitakachompa changamoto nyingi kwenye maisha.
Mbali na kutamani mkwanja, alitaka kuonekana kwenye runinga kubwa za Afrika kwa saa 24, na siku saba kwa kuwa ni mtu anayependa kuonekana kuwa yupo ‘attention.

Anasema anapenda kuangalia runinga na sinema kama
Scarface na watu anaowazimia katika tasnia hiyo ni Al Pacino na Mos Def
wa mtoni. Anakula chochote isipokuwa kitimoto. Kitabu anachokipenda ni
48 Laws of Power.
ANATAKA KUWA KAMA OBAMA
Sehemu anayoipenda Kenya ni Nairobi na haijalishi ni Kaskazini au Kusini ilimradi tu nyumbani ni nyumbani. Anatamani awe kama Rais Barack Obama wa Marekani kwa sababu anajiamini mwenyewe na anaweza kufanya kilichoshindikana kikawezekana kutokana na ushawishi alionao.
MAISHA YA MAPENZI
Katika masuala ya kimapenzi CMB Prezzo amekuwa gumzo kwa kipindi chote cha ustaa wake na mengi yamekuwa yakisemwa.
PREZZO NA SHEILA
Tukiacha huko nyuma akiwa mtoto wa vitoto, Prezzo aliwahi kugeuka gumzo baada ya kutoka na msichana mrembo wa Kenya, Sheila Mwanyigha ‘Nikki’.

Ni
kweli wawili hao walidumu kwa muda mrefu huku wakitoka ‘out’ na kwenye
shughuli mbalimbali wakitumia msafara wa magari ya gharama kama
Limousine, yaani kama rais. Kuna wakati ilielezwa kuwa ndiye msanii wa
kwanza kutumia helikopta Afrika Mashariki huku baadhi wakisema kuwa
ilikuwa ya mama yake.
Pamoja na kudumu na Nikki kwa muda mrefu, ghafla ulipita ukimya huku kukiibuka madai kuwa alioa kimyakimya.
Hata
hivyo, alipotangazwa kwenda BBA, kuliibuka habari kuwa ana mwanamke
mwingine aliyetajwa kwa jina la Huddah Monroe ‘The Lady Boss’ ambaye
aliiwakilisha Kenya BBA mwaka huu kabla ya kutolewa wiki ya kwanza.
PREZZO NA GOLDIE
Akiwa mjengoni BBA, Prezzo alidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mshiriki wa Nigeria, Mwanamuziki Goldie aliyekutwa na umauti siku chache baada ya kumalizika kwa shindano hilo huku kukiwa na taarifa kuwa wawili hao walipanga kufunga ndoa ‘soo’.
PREZZO, DIVA NA THE LADY BOSI
Siku chache baada ya Goldie kufariki dunia, Prezzo alitimba Bongo kwa sababu ni rafiki mkubwa wa akina Ambwene Yessayah ‘AY’ ndipo kukaibuka madai kuwa alinasa kwenye penzi la Loveness Malinzi ‘Diva’ wa Clouds FM.

Kukawa na maneno mengi, Diva akapata ‘kick’ kwenye vyombo vya habari Afrika Mashariki na kwingineko.
Wakati
hayo yakiendelea, hivi karibuni kuliibuka ‘drama’ nyingine. Safari hii
The Lady Boss aliibuka na kudai kuwa Diva amemnyang’anya tonge mdomoni
hivyo kuthibitisha kuwa pamoja na ukongwe, Prezzo naye ni sukari ya
warembo!

Post a Comment