BUFFON AOKOA PENALTI TATU IKIWEMO YA FORLAN KUIPA ITALIA USHINDI WA TATU KOMBE MABARA.
KIPA
Gianluigi Buffon amekuwa shujaa wa Italia usiku huu baada ya kuokoa
michomo mitatu ya penalti na kuiwezesha The Azzurri kutwaa nafasi ya
tatu katika Kombe la Mabara baada ya kuifunga Uruguay kwa penalti 3-2.
Timu hizo zilitoka sare ya 2-2 baada ya dakika 120 huku Italia wakitengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga.
Davide Astori aliwafungia Wataliano bao la kuongoza dakika ya 25 kabla ya Edinson Cavani kusawazisha dakika ya 58.
Shujaa: Gianluigi Buffon ameokoa penalti tatu
Alessandro
Diamanti akaifungia bao la Italia dakika ya 73, kabla ya Cavani
kusawazisha tena 78 na mchezo kuhakia katika muda wa nyongeza, ambako
ilishuhudiwa Riccardo Montolivo akitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya
kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.
Kisha Buffon akaokoa mikwaju ya Diego Forlan, Martin Caceres na Walter Gargano kuipa ushindi Italia.
Alberto Aquilani, Cavani, Stephan El Shaarawy na Suarez wote walifunga kabla ya Mattia De Sciglio kukosa.
Caceres akakosa na Emanuele Giaccherini akafunga kabla ya Buffon kuokoa mkwaju wa Gargano.
Kikosi
cha Italia kilikuwa: Buffon, Maggio, Chiellini, Astori/Bonucci dk96, De
Sciglio, Candreva, De Rossi/Aquilani dk70, Montolivo,
Diamanti/Giaccherini dk82, Gilardino na El Shaarawy.
Uruguay: Muslera,
Caceres, Lugano, Maxi Pereira/Pereira dk81, Godin, Gargano,
Rodriguez/Gonzalez dk56, Arevalo Rios/Perez dk106, Forlan, Suarez na
Cavani.
Washindi wa tatu: Italia wakisherehekea kuifunga Uruguay
Namba 1: Buffon akiokoa penalti ya kwanza ya Uruguay iliyopigwa na Diego Forlan
Na tena: Kisha akaokoa ya Walter Gargano

Post a Comment