AMANDA, BWANA MISOSI WAMWAGANA.
HATIMAYE wale wapenzi waliong’aa hivi karibuni, mwigizaji Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda’ na Mbongo Fleva, Joseph Rushahu ‘Bwana Misosi’ wanadaiwa kumwagana rasmi.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Amanda ili aelezee ukweli kuhusu habari hizo ambapo alikiri kuwa ni kweli wameshaachana na hii ni baada ya kushindwana kitabia.
Tamrina Mohamed Poshi ‘Amanda.
“Mimi na (Bwana) Misosi tumeachana muda mrefu tangu mwezi wa pili
baada ya kushindwana na katika uhusiano wa kimapenzi, nimejifunza kuwa
wanaume siyo watu wa kuwaamini asilimia mia moja kwani baadaye unaweza
kujuta,” alisema Amanda.Kwa upande wake Bwana Misosi hakuweza kujibu moja kwa moja swali aliloulizwa bali alianza kwa kujikanyagakanyaga
“Kwanza niko safarini, je, ni nani aliyekuambia hizo habari….hebu ngoja nimpigie huyo Amanda nimuulize nani aliyetoa siri hiyo,” alisema Misosi.
CREDIT: GLP
Post a Comment