Homa ya Uti wa mgongo(Meningitis).
Homa ya uti wa mgongo hutokea iwapo utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo utapatwa na maambukizi.
Ugonjwa wa Uti wa mgongo husababishwa na nini?
Ugonjwa huu husababishwa na vimelea mbalimbali vya makundi ya bakteria,
virus na hata fungus.
Tukivigawanya visababishi hivi katika makundi haya, tutaona kuwa bakteria wanaosababisha ugonjwa wa uti wa mgongo ni kama vile; bakteria wajulikanao kama Beta-streptococci, Hemophilus influenza, Escherichia coli, Listeria monocytogenes, Neisseria meningitides, Streptococci pneumoniae pamoja na Mycobacteria tuberculosis, ambao pia ni maarufu kwa kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.

Aidha kutoka kundi la virus, virus wanaojulikana kwa kusababisha ugonjwa
huu wa uti wa mgongo ni pamoja na Herpes simplex type 2, HIV pamoja na
Varicella zoster.
Vimelea vya fungus ambavyo hujulikana kwa kusababisha ugonjwa wa uti wa
mgongo ni pamoja na wale wajulikanao kama Coccoidiodomycosis pamoja na
Cryptococci meningetides.
Habari na www.paulmasua.com
Dalili za ugonjwa wa uti wa mgongo
Dalili na viashiria vya uti wa mgongo ni pamoja na
Shingo kukakamaa na kuwa ngumu isivyo kawaida
Mgonjwa kujihisi homa kali
Maumivu makali ya kichwa
Mgonjwa kupoteza fahamu
Mgonjwa kupatwa na degedege (seizures) na mwili kukakamaa
Mgonjwa kushindwa kuvumilia mwanga (photophobia)
Mgonjwa kutoweza kukaa sehemu yenye makelele (phonophobia)
Kwa watoto, kuvimba utosi

Aidha, wakati wa kumfanyia mgonjwa uchunguzi, daktari anaweza kuangalia
pia viashiria vingine vinavyoonesha kuwepo kwa ugonjwa wa uti wa mgongo.
Ishara hizi ni kama vile
Mgonjwa uhisi maumivu kwenye uti wa mgongo yanayozuia kukunjua goti
wakati anapofanyiwa uchunguzi wa kukunjua goti lake (pain limits passive
extension of the knee). Ishara hii huitwa ishara ya Kerning au
Kerning's sign.
Wakati mwingine mgonjwa anapoelekezwa kujitahidi kukunja shingo, miguu
(yaani paja pamoja na goti) navyo hujikunja pia (flexion of the neck
causes involuntary flexion of the knee and hip). Ishara hii huitwa
ishara ya Brudzinski au Brudzinski’s sign.
Vipimo na uchunguzi
Pamoja na kumchunguza mgonjwa kuhusu kuwepo kwa dalili na viashiria vya
ugonjwa huu wa Uti wa mgongo, daktari pia anaweza kufanya vipimo
vifuatavyo;
Kuchunguza damu ya mgonjwa kwa ajili ya kuangalia uwepo wa vimelea
vinavyosababisha ugonjwa na pia kufahamu ni aina gani ya vimelea hao.
Hali kadhalika, damu inaweza pia kutumika kuotesha vimelea maabara ili
kugundua aina ya vimelea na dawa gani nzuri zinazofaa kwa ajili ya
matibabu (culture and sensitivity).
Kipimo kinachofanyika kwa kuchukua maji ya uti wa mgongo wa mgonjwa na
kuyachunguza maabara ili kutambua uwepo wa vimelea, aina ya vimelea na
dawa zinazofaa kutibu vimelea hao (Lumbar puncture).
Kwa baadhi ya maeneo yenye vifaa kama CT-scan na MRI, mgonjwa pia huweza kuchunguzwa kwa kutumia vifaa hivi ili kufahamu uwepo wa ugonjwa, sehemu lilipo na madhara yaliyosababishwa na ugonjwa huu wa uti wa mgongo. Hata hivyo vipimo hivi haviwezi kutambua aina wala dawa ya kutibu vimelea vinavyosababisha ugonjwa huo.

Matibabu ya ugonjwa wa Uti wa Mgongo
Kwa wagonjwa waliopoteza fahamu ni vizuri kuhakikisha wanapumua vizuri,
na njia za hewa ziko wazi. Halikadhalika, iwapo itathibitika kuwa
bakteria ndiyo wanaosababisha ugonjwa huu, mgonjwa anaweza kupewa
mojawapo ya dawa hizi za antibiotiki kama cefotaxime au Cefriaxone.
Aidha baadhi ya madaktari hupendelea kuongeza dawa za steroids kama
dexamethasone kama sehemu ya matibabu.
Iwapo itathibitika ugonjwa huu umesababishwa na virus, dawa kama
Acyclovir huweza kutumika. Hali kadhalika, ikithibitika kuwa vimelea
waliosababisha ugonjwa huu ni wa kundi la fungus, dawa kama Amphotericin
B au flucytosine zaweza kutumika. Mgonjwa pia hupewa Paracetamol kwa
ajili ya kushusha homa na kuondoa maumivu ya kichwa.
Madhara yanayoweza kuletwa na ugonjwa wa uti wa mgongo
Ugonjwa wa uti wa mgongo unaweza kusababisha
Kuamshwa kwa chembechembe za damu zinazo sababisha damu kuganda kitaalamu – Disseminated Intravascular Coagulopathy (DIC).
Kuvuja damu kwa katika tezi za adrenalin na kupelekea kutokea kwa ugonjwa ambao kitaalamu unaitwa – waterhouse friderichsen syndrome.
Kwa watoto, ugonjwa huu unaweza kusababisha mtoto kuwa na kichwa kikubwa - hydrocephalus.

Post a Comment