HATIMAYE MANCHESTER UNITED KUBADILI NYASI MBOVU ZA OLD TRAFFORD BAADA YA MIAKA 10- SHAFFIH DAUDA.
![]() |
| Shaffih Dauda, Ismail Sota, tour guide wa Old Trafford, na Jonstone Mulunda |
Habari na Shafiih Dauda.
Siku
ya jana nikiwa bado hapa nchini Uingereza nilifanikiwa kufanya ziara
kwenye uwanja wa pili kwa ukubwa hapa UK - uwanja wa Manchester United -
Old Trafford.
Katika ziara yangu ya leo kwenye makao makuu ya klabu ya Manchester United nimefanikiwa kujifunza vitu vingi sana, na kwa utaratibu nitaanza kuwajuza wapenzi wasomaji wa mtandao huu.
UWANJA WA OLD TRAFFORD - SEHEMU YA KUCHEZEA
Katika ziara yangu ya leo kwenye makao makuu ya klabu ya Manchester United nimefanikiwa kujifunza vitu vingi sana, na kwa utaratibu nitaanza kuwajuza wapenzi wasomaji wa mtandao huu.
UWANJA WA OLD TRAFFORD - SEHEMU YA KUCHEZEA
![]() |
| Nikiziaga nyasi za Old Trafford ambazo zinatarajiwa kuondolewa |
Katika kipindi cha hivi karibuni sehemu ya kuchezea ya uwanja Manchester United imekuwa ikalalamikiwa kwamba haina ubora mzuri. Kufuatiwa malalamiko hayo uongozi wa Manchester United umeamua kubadilisha nyasi za sehemu ya kuichezea za uwanja zilizodumu kwa takribani miaka 10 sasa.
Uwanja huo ambao United walianza kuutumia mnamo mwaka 1910 ndio uwanja wa tisa wa ukubwa barani ulaya wenye uwezo wa kuingiza watu 75,765, katika miaka ya hivi karibuni umekuwa ukichezewa mechi za mchezo wa Rugby tangu mwaka 1998, mechi ambazo zimepelekea uharibifu mkubwa wa sehemu ya kuchezea ya Old Trafford.
![]() |
| Timu ya watoto wa Manchester United |
Uwanja huo kwa sasa unachezewa na timu ya watoto ya Manchester United baada ya msimu wa ligi kumalizika, na sasa unatarajiwa kuanza kufanyiwa marekebisho baada ya mechi ya magwiji wa klabu ya Manchester United dhidi ya wale wa Real Madrid itakayofanyika siku ya jumapili wiki hii.
Gharama za marekebisho ya nyasi mpya zinazotarajiwa kuwekwa kwenye uwanja huo wa Old Trafford zina gharama ya £250,000, na ukarabati wa huo utaanza rasmi siku ya jumatano.
Habari na Shaffih Dauda



Post a Comment