Papa Francis aja Mei 6 Mwaka huu
KIONGOZI mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa
Francis I, ameichagua Tanzania kuwa nchi yake ya kwanza
atakayoitembelea mwezi Mei mwaka huu tangu achaguliwe kushika wadhifa
huo.
Ziara ya Papa Francis I itaiweka Tanzania katika historia ya dunia kwa kutembelewa na kiongozi huyo mkubwa wa Kanisa Katoliki ikiwa ni mara ya pili baada ya hayati Papa Yohane Paul II kufanya ziara kama hiyo mwaka 1990.
Taarifa iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC) jana jijini Dar es Salaam ilisema kuwa Papa Francis I ambaye amechukua mikoba ya Papa Benedict XVI aliyejiuzulu, atawasili nchini Mei 6 kwa ziara ya siku nne.
Akiwa nchini, Papa Francis I mwenye umri wa miaka 76 atakutana kwa mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete Ikulu, kisha kuongoza ibada ya misa katika Uwanja wa Taifa na kutembelea mikoa ya Arusha, Mwanza na Mbeya.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa akiwa katika mikoa hiyo, atakutana na waumini katika ibada za misa ikiwa ni pamoja na kutoa sakramenti za kipaimara na daraja takatifu la upadrisho.
TEC ilisema kuwa Papa ataondoka nchini Mei 10 kuelekea nchini Uganda ambako atakuwepo kwa siku tatu, kisha ataelekea katika mataifa ya Ghana na Afrika Kusini na baadaye kuelekea nchini kwao Argentina.
Waumini wa Kikatoliki pamoja na wale wa madhehebu mengine wamesisitizwa kutoizingatia taarifa hii kwani LEO NI SIKU YA WAJINGA DUNIANI.
CHANZO TANZANIA DAIMA

Post a Comment