ad

ad

Omotola aelezea mapenzi yake kwa mumewe

NDOA ya muigizaji maarufu wa Nollywood, Omotola Jelade Eleinde imetimiza miaka 17, ikiwa na mafanikio makubwa.
 

Uhusiano wao umezidi kuimarika siku hadi siku na hivyo ndoa hiyo kuwa ya mfano kwa vijana wengi.
 
Kwenye sherehe maalum ya kumbukumbu ya ndoa yao, Omotola hakusita kutoa ujumbe maalum kwa mume wake mpenzi Rubani Matthew Ekeinde Tafadhali naomba nichukue muda mchache kumuelezea huyu mwanaume. Hapa duniani kuna wavulana na kuna wanaume. 

Wewe ni mwanaume, Kapteni Matthew Ekeinde. Baba yangu alifariki nikiwa binti wa pekee, nilihitaji mwanaume kwenye maisha yangu. Ulikuja, umekuwa baba, mwalimu, rafiki na mwenza mwaminifu
 
Akizungumza kwa bashasha katika siku hiyo ambayo pia ilikuwa ni maalum kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa mume wake, Omotola hakusita kumshukuru Mungu kwa neema aliyomjalia kwa kumpa mwanaume wa maisha yake.

 Tumeishi pamoja kwa kipindi kirefu, tumekuwa tukiamini pamoja, mwanaume unayemuogopa Mungu, umekuwa ukinifundisha njia za kumuabudu Mungu leo hii nimesimama vizuri katika hilo, alisema
 
Miaka 17 iliyopita kwenye siku yako ya kuzaliwa tulifunga ndoa. Unakumbuka imekuwa kama jana tu! Mume bora, baba bora na rafiki bora. Mungu akupe maisha marefu
Powered by Blogger.