Habari zaidi, viongozi wa kutoka
mataifa ya Latin Amerika, wamekuwa wakituma pongezi zao kwa Papa mpya
mteule wa kanisa Katoliki Francis 1. Papa huyo anatokea nchi ya
Argentina, na anakuwa Papa wa kwanza kutoka sehemu hiyo.
Pongezi nyingi kumiminiwa Papa mpya

Rais wa Argentina
Argentina, ikiwa ndio asili ya Papa, ilikuwa na
sababu kubwa zaidi kusherehekea uteuzi wake. Licha ya uhusiano wa
msuguano kati ya rais wa Argentina, Christina Fernandez, alikuwa wa
kwanza kutuma pongezi kwa Papa Francis, huku akimtakia kila kheri katika
kupigania haki na usawa.
Wawili hao waliwahi kutofautiana hadharani juu ya suala la ndoa ya watu wa jinsia moja.

Rais wa Brasil Dilma Rousef atuma pongezi kwa Papa
Nchini Brasil, inayotazamiwa kuwa na idadi kubwa
zaidi ya waumini wa kanisa hilo la Roma duniani, rais Dilma Rousef
alimpongeza sana Papa Francis, na kwa jumla wananchi wa Argentina. Pia
alimkaribisha Papa Francis kwa moyo mkunjufu kuhudhuria sherehe za
kuadhimisha siku ya vijana duniani mnamo Julai, mjini Rio.

Bendera ya Chile
Kwa rais wa Chile, Sebastian Pinera alisema kuwa
ameridhishwa na kuwa Papa huyo mpya anaielewa nchi ya Chile vizuri sana
na hata akamkaribisha kuja kuzuru tena.

Bendera ya Colombia
Rais wa Colombia Juan Manuel Santos, yeye
alifurahishwa zaidi na kuwa kwa Mara ya Kwanza wamepata Papa ambaye
lugha yake ya mama ni Kispania.
Post a Comment