"VIDEO YA LWAKATARE NI FEKI" HII NI KAULI YA DR. SLAA
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa amezungumzia video aliyorekodiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare na kusema ni ya kutungwa na vyombo vya dola.
Dk. Slaa pia amelituhumu Jeshi la Polisi kufanya mchezo mchafu kwa maslahi ya kisiasa.
HII NDO VIDEO ILIYOZUA UTATA...
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho kufafanua suala la kushikiliwa kwa Lwakatare.
Dk. Slaa, alilalamikia jeshi la polisi kuwa limekuwa likitumika kisiasa
huku akitoa mfano wa chama hicho kuwa kimekuwa kikitaarifu jeshi la
polisi kuhusu mambo hayo lakini halijawahi kuchukua hatua.
Alisema jeshi la polisi halijawahi kuchukua hatua stahiki kwa suala la
mauaji ya Daudi Mwangosi kumwajibisha Kamanda wa polisi wa Mkoa wa
Iringa aliyesimamia na kufanikisha kifo cha mwandishi huyo wa habari,
jeshi la polisi pia halikuchukua hatua za kumhoji Dk. Stephe Ulimboka
baada ya kuteswa na mtu anayedaiwa kuwa ni Afisa wa usalama wa Taifa wa
Ikulu, hali kadhalika hawezi kushangaa ikiwa jeshi la polisi halitaacha
kumhoji Absalom Kibanda.
Amesema, jeshi la polisi limekuwa likitoa taarifa za kukichafua chama,
akikumbushia suala la Mwangosi, alisema kuwa mara tu baada ya tukio la
Mwangosi kuuawa, jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wake lilitoa
taarifa kuwa alilipuliwa na kitu kilichorushwa kwake akikimbilia
kujisalimisha kwa polisi akitoka kwa wafuasi wa Chadema, jambo ambalo
lilikuwa sio kweli.
Hivyo alisema, Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa Chama hicho
kuhusishwa kwa sakata la sasa la mkanda wa video uliopo katika mtandao
na Kibanda ni mwendelezo tu wa kukihujumu chama, unaoratibiwa na Usalama
wa Taifa, huku ukitekelezwa na jeshi la polisi.
“CHADEMA kinafahamu kwa undani, kwamba uzushi huu wa Tape ya “Bukoba
Boy”.Tunajua huu umeanzishwa na kuhusisha Usalama wa Taifa, akiwemo
Ighondo na wenziwe pale Ada Estate. Huyu Ighondo ambaye anafahamika pia
kwa jina la “Rama” tunamfahamu vizuri sana," alisema
Dk Slaa aliingiza suala la kufungiwa suala la kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi akiituhumu serikali kutokua makini.
Akakumbushia kuwa waliwahi kutuma barua mbalimbali polisi
zinazothibitisha kuwa wanafanyiwa michezo michafu huku zikiwa
zimeandikwa majina ya viongozi wa CHADEMA, au taarifa za Vikao vya
Chadema zilizopotoshwa lakini polisi hawakuchukua hatua.
Aliongeza kuwa wakati wa uchaguzi wa Igunga walisema kuwa kuna mtu
anamiliki bastola isisvyo halali, wakataja hadi namba za bastola
iliyoingizwa lakini polisi hawajawahi kushughulika nayo.
Hata hivyo alishangazwa na jeshi la polisi kufanya haraka kumshikilia
Lwakatare, kwani vyombo vya habari hivi majuzi vimemtaja kwa majina ya
watu kuhusishwa na utekwaji na uteswaji wa Kibanda, lakini jeshi
halikusema lolote hadi sasa.
Akaongeza kuwapo watu aliowataja kwa majina kwamba waliingia kwa ID zao
kwenye mitandao kukejeli suala la kuteswa Absalom Kibanda lakini jeshi
halikuchukua hatua.
Alishangazwa jinsi polisi walivyofanya haraka kumkamata Lwakatare, akasema ni mbinu tu za kukichafua CHADEMA.
Hadi tunaenda Mitamboni, Jeshi la polisi lilikuwa halijatoa taarifa
kuwa Mkurugenzi huyo wa Ulinzi na usalama wa Chadema angepata dhamana au
la, lakini Wakili wake alilithibitishia gazeti hili kuwa wameenda tena
kumpekua kwa mara nyingine nyumbani kwake.
Kutokana na hali hiyo, Dk Slaa alisisitiza kuwa “madai yaliyotolewa
mara nyingi na CHADEMA, kwa Rais kuandikiwa barua na Mwenyekiti wa
Chadema Freeman Mbowe, iundwe Judicial Commission of Inquiry (Tume Huru
ya Kimahakama kuchunguza vifo vyote vyenye utata na sura ya kisiasa).
Akahoji ,Serikali inaogopa nini kuunda Tume hii huru ili ukweli
Ujulikane? Iweje CHADEMA inayotuhumiwa Kupanga njama wanaishinikiza
Serikali kuunda Chombo huru na Serikali ndiyo inayopata kigugumizi?”
Aliongeza kuwa “kwa wale walioumizwa na kujeruhiwa kama kina Ulimboka
Kibanda na wengine, tunarudia Tamko letu la kuwa hatuna Imani na
uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwa viongozi wa Jeshi hilo
ni sehemu ya watu tunaowatuhumu kwa kuhusika kwa njia mbalimbali, na
Ushihidi wa wazi na Taarifa mbili za Serikali kupingana yaani Taarifa ya
Kamati ya Nchimbi na Tume ya Haki za Binadamu.
"Tutaiaminije Polisi na Serikali kwa Taarifa ya Kamati ya Nchimbi?
Hatuwezi kuendelea kuvumilia ukandamizaji huu wa uhuru wa habari, ambao
sasa unaelekea kuota mizizi nchini kwetu.
Na kweli ninawaomba na
kuwataka waandishi wote msimame imara, bila kujadili itikadi, au tofauti
zetu zozote zile na kusimamia uhuru wa Habari.
Tunataka vivyo hivyo,
kwa wanaharakati mbalimbali. Waache hofu, eti wanaogopa kuhusishwa na
vyama vya Siasa! Haki ni haki na haina rangi ya bendera ya chama
chochote," alisema.
Azungumzia Bunge:
Dk Slaa amesema kuwa usalama wa Taifa, unafanya kazi kwa maslahi ya Chama cha Mapinduzi hadi ndani ya bunge, ndio maana sasa wabunge wa Chama hicho wameondolewa katika kamati muhimu ambazo walikuwa wanazisimamia, bila wao kuulizwa, tofauti na walivyojaza katika fomu na nje ya ushauri wa Kiongozi wa upinzani bungeni.
Dk Slaa amesema kuwa usalama wa Taifa, unafanya kazi kwa maslahi ya Chama cha Mapinduzi hadi ndani ya bunge, ndio maana sasa wabunge wa Chama hicho wameondolewa katika kamati muhimu ambazo walikuwa wanazisimamia, bila wao kuulizwa, tofauti na walivyojaza katika fomu na nje ya ushauri wa Kiongozi wa upinzani bungeni.
Dk slaa alisema hiyo yote ni hujuma, Mnyika amepelekwa Ardhi maliasili
na Mazingira, huku Msigwa akiondolewa maliasili na utalii kwa kuwa
alikuwa anawataja viongozi wa CCM , jeshi la Polisi, jeshi la Wana
nchina Ikulu yenyewe kuhusishwa na ujangili wa wanyama.
Amesikitishwa na wabunge wa Chama chake kuhamishwa kamati muhimu
walizokuwa wanazisimamia, huku wengine wakiachwa kuingizwa katika kamati
jambo ambalo linawanyima ufuatiliaji wa utendaji wa serikali, ilihali
wabunge wengi wa CCM wengine wamewekwa kamati mbili kwa mbunge yule
yule.

Post a Comment