DIAMOND AMPA PENNY GARI LA KWENDEA CLINIC, AMUAGIZIA JINGINE JIPYA
Habari ni kuwa Mwanamuziki Diamond Platinumz na mpenzi wake ambaye pia
ni presenter Penny wanatarajia kupata mtoto. Kupitia U Heard ya
XXL(Clouds fm) Diamond ambaye tayari anakubalika nchi kadhaa kimuziki
amesema kuwa amempa Penny gari la kutembelea na pia amemuagizia jingine
jipya aina ya Hyundai ix35 ili limsaidie kwenda clinic. "That's true, ni
kweli unajua sitaki kusema ni mpenzi wangu, sasa hivi ni mama watoto
wangu kwa sababu ya mizunguko ya kwenda clinic na nikaona sio vizuri
kwenda kwenye madaladala kugombania......nikaona ni vizuri nikimnunulia
gari ya kwendea na vitu vingine. Nimemuagizia ile new model ya Hyundai
ix35" . Penny mwenyewe amezidi kuwa mrembo na kuanza kunenepa kuonyesha
kuwa kazi aliyoifanya Diamond imekubalika.
Hongera sana kwa wawili hao.
Hongera sana kwa wawili hao.

Post a Comment