Pengo: Polisi ni tatizo - KUUAWA PADRI EVARIST
KANISA Katoliki nchini, limesema limesikitishwa na usiri unaofanywa
na Jeshi la Polisi kushughulikia matatizo mazito, yakiwamo mauaji ya
Padri Evarist Mushi aliyepigwa risasi na watu wasiofahamika kisiwani
Zanzibar, Februari mwaka huu.
Kardinali Pengo
Mbali ya mauaji hayo, kanisa hilo pia limesema linasikitishwa kuona
tangu kujeruhiwa Padri Ambrose Mkenda wa Kanisa Katoliki Mpendae, hakuna
chombo cha dola kilichotoa majibu ya kuridhisha dhidi ya upelelezi
unaofanywa.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo, alisema usiri huo hauwezi kuleta matunda yoyote.
Alisema hadi sasa, si yeye wala Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Mhashamu Augustino Shayo waliopewa taarifa za maendeleo ya upelelezi wa matukio yote.
“Mimi nadhani vyombo vya usalama ukimya wao hausaidii kumaliza tatizo lililopo sasa, tukio la mauaji ya padri wetu Zanzibar na lile la kujeruhiwa Padri Mkenda, hadi leo mambo yanaendeshwa kwa usiri, si mimi Kardinali Pengo wala mwenzangu Askofu Shayo anayefahamu kinachoendelea… hali hii haiwezi kusaidia kuimarisha amani nchini, inaonyesha kama vile mambo haya yanataka kufunikwa,” alisema Kardinali Pengo.
Akizungumzia hali ya amani nchini, Kardinali Pengo alisema kuna kila sababu Serikali kuona umuhimu wa kukutana na viongozi wa dini za pande zote ili kujadiliana.
Alisema hali ya kutoelewana kama ikiachwa ikiendelea hivi, taifa litakuwa katika hatari kubwa.
“Kama ni suala la udini, mbona tumeishi kama ndugu kwa muda mrefu, hapa huenda kuna kitu kimejificha,

sisi kama viongozi tunawajibu wa kukutana
na kujadiliana, Serikali ndiyo ina wajibu mkubwa wa kuona hali hii si
njema na kuna kila sababu ya kutafuta chanzo na suluhu,” alisema Pengo.
Alisema katika majadiliano hayo, ni vyema pande zote zikakubali kufikia muafaka badala ya kufanya malumbano ambayo yatakuwa hayana tija yoyote kwa taifa.
Alipoulizwa kuhusu fununu za watu wasiofahamika kuvamia makanisa katika mkesha wa Sikukuu ya Pasaka, Kardinali Pengo alisema yeye binafsi kazi yake ni kuwaimarisha kiroho wananchi na hawatumii silaha, hivyo jukumu la kuimarisha usalama ni la Serikali.
“Mimi binafsi, sioni sababu za kushindwa kwenda kusali kanisani kutokana na tishio la kuvamiwa makanisani, ninachoahidi hata kama nikisikia kuna watu wanataka kuja kuniua nikienda, nitakwenda na kuingia ili mradi nife nikiomba,” alisema Kardinali Pengo.
Hata hivyo, Pengo alitumia fursa hiyo kumtahadharisha kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I kutokana na mazingira anayoishi.
Alisema dunia ya sasa imebadilika mno na anapaswa kuishi kwa kuchukua tahadhari.
“Papa amezoea kuishi maisha ya kawaida ya kuwa jirani na jamii, lakini kutokana na mazingira yetu nafikiri ni muda muafaka sasa wa kubadili maisha haya na kuchukua tahadhari,” alisema Kardinali Pengo.
Alisema lengo kuu la Papa Francis I kuishi hivyo, kunatokana na kupambana na wakandamizaji ambao wanawanyima haki za msingi watu masikini, watu wanaowakandamiza masikini na fukara,” alisema Pengo.
Alisema hali ya uvunjifu wa amani inaweza kutokea wakati wowote, kama vila ambavyo iliwahi kumkuta marehemu Papa John Paul II, ambaye alipigwa risasi na kujeruhiwa.
Kuhusu mchakato wa kumpata Papa mpya, alisema ulifanyika kwa amani tofauti na watu wengi wanavyofikiri.
“Ukiwa mle ndani, haufahamu vinavyoendelea nje lakini ninachofahamu mimi hata mwizi akipanga kuiba hujiandaa, hivyo hata yule mtu anayedaiwa alivamia mkutano wetu angejiandaa hata kwa mavazi yanayofanana na sisi tu, huenda amechanganyikiwa,” alisema Pengo.
Katika hatua nyingine, Kardinali Pengo amewatakia Watanzania Sikukuu ya Pasaka njema, huku akisisitiza ujumbe wa mwaka huu ni; “Tujenge amani, mshikamano na upendo” na kwamba itafanyika kitaifa mkoani Dodoma.

KUUAWA PADRI EVARIST
Padri Evarist Mushi alifariki dunia, baada ya kupigwa risasi utosini na watu wasiojulikana.
Padri huyo, alikuwa akielekea kanisani kuendesha misa ya saa 3 asubuhi, kwenye Kanisa la Mt. Theresia.
Tukio hilo, lilitokea eneo la Mtoni ambapo alisimamishwa na watu wawili ambapo mmoja wao alimpiga risasi utosini na kufariki papo hapo.

CHANZO NI GAZETI LA MTANZANIA LA LEO MACHI 28,2013

Post a Comment