ad

ad

ICC yamfutia mashtaka Francis Muthaura wa Kenya

Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imefuta kesi iliyokuwa ikimkabili mkuu wa zamani wa utumishi wa umma nchini Kenya, Francis Muthaura kwa madai ya kukosekana ushahidi wa kutosha.
Mwendesha mashtaka wa ICC, Bi. Fatou Bensouda amesema mashahidi muhimu kwenye kesi hiyo wamejiondoa na hivyo kudhoofisha kesi yenyewe. Muthaura alikuwa akikabiliwa na tuhuma za kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007. Francis Muthaura alikuwa miongoni mwa Wakenya 4 wanaokabiliwa na kesi za jinai dhidi ya binadamu mbele ya mahakama hiyo yenye makao yake mjini Hague, Uholanzi.

Mkuu huyo wa zamani wa utumishi wa umma alikuwa kwenye kundi moja na Rais Mteule, Uhuru Kenyatta. Watuhumiwa wengine ni Makamu wa Rais mteule, William Ruto pamoja na mtangazaji wa radio, Joshua Arap Sang. Kesi ya Sang na Ruto inatarajiwa kuanza mwezi Mei huku ile ya Kenyatta ikitarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.
Weledi wa mambo wanasema huenda ikawa vigumu kwa Kenyatta na Ruto kuhudhuria vikao vya ICC hasa baada ya kuchaguliwa Rais na Makamu wa Rais siku chache zilizopita.
Powered by Blogger.