ad

ad

Makao makuu ya soka Misri yateketezwa moto

Waandamanaji waliokuwa na hasira wameteketeza moto makao makuu ya Shirikisho la Soka Misri mjini Cairo.
Aidha mtu moja anaripotiwa kuuawa baada ya kupigwa risasi na vikosi vya polisi karibu na Medani ya Tahriri mjini Cairo.
 Machafuko hayo yameibuka Jumamosi baada ya Mahakama ya Jinai Cairo kuidhinisha  hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi ya watu 21 mwaka 2012 katika kesi ya machafuko yaliyojiri baada ya mechi ya soka mjini Port Said. Mahakama hiyo pia ilitoa hukumu ya kifungo cha maisha dhidi ya watu wa tano. Waliohukumiwa wamepatikana na hatia ya kuwaua watu 74 katika ghasia zilizoibuka mjini Port Said baada ya timu ya mji huo, Al-Masry kuifunga Al 

Ahly ya Cairo mabao matatu kwa moja mapema mwaka 2012. Wakaazi wa Port Said wamekasirishwa na hukumu ya mahakama iliyowapata na hatia wakaazi wa mji huo. Maandamano yameripotiwa katika mji huo wa Mfereji wa Suez na tokea Machi 3  ambapo watu wapatao saba wameuawa. Wamisri wanasema hukumu iliyotolewa na mahakama ni ya kisiasa na inaipendelea timu ya Al Ahly ambayo ni kati ya timu zenye ushawishi mkubwa zaidi nchini Misri.
Powered by Blogger.