ad

ad

Marais wa Iran na Pakistan wazindua bomba la gesi

Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mwenzake wa Pakistan Asif Ali Zardari wamezindua rasmi awamu ya kwanza ya ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi utakaogharimu mabilioni ya dola.
 Marais hao wawili wamehudhuria hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika mpakani  mwa nchi mbili na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Mafuta wa Iran Rostam Qasemi na Waziri wa Mambo ya 

Nje Ali Akbar Salehi. Bomba hilo litasafirisha gesi asilia kutoka Iran kuelekea nchini Pakistan na viongozi wa nchi hizi mbili wamesema kuwa mradi huo utaimarisha amani, usalama na maendeleo ya Iran, Pakistan pamoja na mataifa mengine ya eneo hili.
Bomba hilo la gesi litakalokuwa na urefu wa kilometa 1,600 litapunguza uhaba wa nishati nchini Pakistan kwa kusafirisha kila siku mita mraba milioni 21.5 za gesi asilia ya Iran hadi Pakistan.
Powered by Blogger.