HACKERS WAIBA TAARIFA ZA KIFEDHA ZA MICHELLE OBAMA
Hackers ni watu wajanja wajanja wa
mitandaoni ambao huweza kuiba taarifa mbalimbali za siri za watu. Yaweza
kuwa taarifa za kibenki nk.
Hivi karibuni nchini Marekani hackers
wamefanikiwa kuiba taarifa za siri za watu mbalimbali maarufu akiwemo
mke wa Rais Obama, First Lady wa Marekani, Michelle Obama.
Hackers hao wamefanikiwa kuiba na
kuziweka hadharani taarifa za Mrs Obama kuanzia Social Security Number,
taarifa za Credit Cards zake na taarifa zingine binafsi za masuala ya
fedha. Hackers hao wametuma taarifa hizo mtandaoni wakaongeza na ujumbe “
Blame your husband, we still love you, Michelle”….Mlaumu mume wako,
tungali tunakupenda Michelle.
Kwa mujibu wa mtandao wa Gossip Cop,
taarifa binafsi za kifedha za watu maarufu kama vile Beyonce, Kim
Kardashian na hata wanasiasa kama Joe Biden na Hillary Clinton hivi
karibuni zimewekwa wazi katika mitandao
Post a Comment