ad

ad

Dotnata amerudi na moto

MWIGIZAJI wa kike wa filamu ambaye pia ni mtayarisha wa filamu Husna Posh 'Dotnata' anasema kuwa baada ya safari za kutafuta sana Afrika Magharibi amerudi na anataka kuonyesha kile alichojifunza.

"Nimesafiri katika shughuli za kisanaa lakini pia nimejipanga kwa mwaka huu kuzalisha filamu bora kwa kuibua vipaji vipya vyenye uwezo kwa ajili kupanua wigo wa wasanii wachanga ikiwa ni sehemu ya kutengeneza ajira kwa vijana wengi wasio na ajira,"anasema Dotnata.

Dotnata anakuja na filamu yake mpya kwa mwaka huu inayojulikana kwa jina la Subira, aliyowashirikisha wasanii nyota na inamtambulisha msanii Pendo ambaye ni mke wa bondia Japhet Kaseba. Wengine ni Aunt Ezekiel, Baba Haji, Amanda Poshi na Mlawa.
Powered by Blogger.