ad

ad

Mourinho akacha kikao Fifa

Lisbon, Ureno. Kocha wa Real Madrid ya Hispania, Jose Mourinho hakwenda kushiriki kwenye kikao cha tuzo za Fifa Ballon dOr gala kwa vile alionywa kutokwenda na baadhi ya waliompigia kura ya kocha bora wa mwaka, kwa vile waliwapigia kura makocha wengine.

Kutokwenda kwake kwenye kikao hicho kumezua maswali kadhaa miongoni mwa wadau wa soka.
Samahani kwa kushindwa kwenda kwenye kikao cha tuzo za Ballon dOr gala. Ulikuwa uamuzi mzuri kwangu, alisema Mourinho wakati akiongea na kituo cha televisheni cha RTP Jumanne wiki hii katika mahojiano maalum.Nilipokea ushauri kutoka kwa watu wa karibu na mimi. Nimeuzingatia na nimeona heri nisiende kwenye kikao hicho, alisema zaidi Mourinho.
Mtu mmoja, wawili au watatu hivi walinipigia simu na kuniambia kwamba wamenipigia kura, lakini kura hiyo pia amepigiwa mtu mwingine. Hivyo niliamua kutokwenda kushiriki kwenye mkutano huo, alisema.

Kocha huyo Mreno na Kocha wa zamani Barcelona, Pep Guardiola walishindwa kupata tuzo ya Fifa mwaka 2012 baada ya kwenda kwa Kocha wa Timu ya Taifa Hispania, Vicente del Bosque Januari mwaka jana.

Fifa ilisema katika taarifa yake ilisema: Fifa inathibitisha kuwa, orodha ya kura zilizopostiwa kwenye tovuti yake iko sahihi.
Powered by Blogger.