ad

ad

Unasema wa nini, wenzako wanajiuliza watampata lini

MAPENZI ni raha hasa pale unapokuwa na mtu ambaye mna mipango nae katika maisha. Ni mapenzi yasiyofaa na yaliyojaa ujinga kama uko na mtu ambaye hamjui kwanini mmekuwa wapenzi au nini hasa hatma ya uhusiano wenu.

Kwa mfano kukubali kufanya mapenzi na mume wa mtu ni dalili kwamba huenda kichwa chako hakiko sawa, kukubali kufanya mapenzi na mke wa mtu ni kosa kubwa zaidi na lenye kuhatarisha maisha kwa ujumla.

Ndugu zangu ni kweli inawezekana katika maisha yako unasumbuliwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, hata hivyo si sawa hata kidogo kukubali kufanya mapenzi na mume au mke wa mtu eti unategemea akupe fedha au raha fulani.

Waume za watu ni jambo la hatari, zaidi ni kwamba unaingiza mikosi katika maisha yako, kwamba nawe ukiolewa utaibiwa au familia yako itaingia kwenye hali hiyo. Hilo si jambo la kisayansi, lakini ndivyo inavyoaminiwa na wengi. Kama unachezea watoto wa watu, nawe subiri wako atachezewa.

Wanawake wengi kwa mfano wanaona ni sawa tu kuwa na waume za watu hasa kwa sababu ndio wanaongoza kwa kuhonga vitu vya thamani, lakini ukweli ni kwamba watu wanapaswa kubadilika namna wanavyowaza.

Ni lazima katika maisha kutafakari na kuyaangalia maisha kwa mbele zaidi, unapaswa kuwa na mtu ambaye unaweza kuwa na amani naye, hasa pale unapoamua kuoana.

Kuna mabinti wabichi utashangaa kapangishiwa nyumba au chumba na mume wa mtu. Huu ni ujinga ndugu yangu, unahatarisha maisha yako mwenyewe. Mwenye hekima huishi kulingana na hali halisi, si kulazimisha maisha ya raha.

Ni bora kuuza vitumbua au biashara yoyote au jambo lolote la
kukuwezesha kuishi kwa amani, sio kukubali kuishi maisha ya kifahari kwa kumtegemea mume wa mtu.

Kuna wasichana wengine unaweza kuona wakati mwingine wanakwenda mbele zaidi kwa kujengewa nyumba na hata kumvuruga akili mwanaume kiasi cha kusahau kwake.

 
Unamkuta mzee mzima na akili yake, amekuwa mpumbavu, hana muda na watoto wala mkewe, yuko bize na ujinga mitaani.

Kila msichana anayejiremba anataka awe wakendugu yangu kama ni mapenzi huenda umefanya sana, umepata nini tangu uanze kufanya?

Tafakari vizuri. Acha kuendekeza vitu vya hatari na visivyo na tija maishani.

Unasema wa nini, wenzako wanajiuliza watampata lini!
Kuna wengine wamekuwa wakitoleana maneno machafu ndani ya ndoa sababu ni kwamba ana mwingine nje.

Unayemdharau unamuona wa nini amini ninachokwambia kwamba wapo wengine ambao wanajiuliza watampata lini.

Hicho ambacho huenda wewe unakidharau kwa sababu zako ambazo huenda si za msingi, wapo ambao wanatafuta njia ya kufanya ili angalau amshike tu hata mkono.

Kumbuka vizuri wakati mnaanza uhusiano na huyo, alikuwaje? Utakuta kama ni wanawake wengi walikuwa wanavaa vizuri, lakini leo kwa sababu ya mapenzi
yasiyofaa ambayo amepewa, wengine wamejikuta wamejidharau, kiasi kwamba hawaoni tena umuhimu wa kuvaa vizuri.

Jambo la msingi tunapokuwa kwenye uhusiano ni kuacha kudharauliana, badala yake tuwaze namna ya kufanya ili kuboresha mapenzi.

Si vizuri kuwaza kuachana, hata kama kuna migogoro, tuangalie namna ya kuondoa migogoro hiyo.

Kuna watu wamekuwa na mazoea makubwa ya kununa, yaani akikwazana kidogo tu na mwenzake, anachokiona cha maana kwake ni kununa. Mtu mzima hanuni wala hahami kitanda, bali hutafuta suluhu ya tatizo.

Acheni kutunishiana misuli kwamba wewe ni bora zaidi, ndege kutua kwenye mti fulani haina maana kwamba hakuna
miti mingine, bali ni hali tu imetokea, si ndio ndugu yangu?

Powered by Blogger.