AMANDA POSHY NA KING MAJUTO HAPATOSHI NDANI YA NYUMBA NNE.
MWIGIZAJI wa filamu wa kike Bongo Amanda Poshy
amefungua mwaka wa 2013 kwa kuingia na komedi akishirikiana na mwigizaji
mkongwe katika tasnia ya filamu na komedi King Majuto, Amanda ameshiriki katika
Komedi ya Nyumbana nne.
“Nimekamua sana katika komedi na Mzee King Majuto
haikuwa rahisi unajua Majuto anachekesha sana kwa sababu mimi ni msanii
nilionyesha jinsi nilivyokomaa katika kuigiza nikahakikisha nakwenda sambamba
na Mzee Majuto na kuifanya kazi hiyo kuwa ya ukweli,”anasema Amanda.
Filamu ya Nyumba nne King Majuto anajikuta akiwa
katika wakati mgumu baada ya kuoa wanawake wanne na kila mwanamke ana tatizo
lake King Majuto anajikuta akiwa na matatizo na kuwa mtu kati mwenye kutatua
matatizo kila kukicha, hiyo ndio komedi ya Nyumba nne.
Msapoti kwa kulike page yake Amanda Poshy link hii hapa bofya hapa www.facebook.com/pages/Amanda-Poshy-Fanpage
Msapoti kwa kulike page yake Amanda Poshy link hii hapa bofya hapa www.facebook.com/pages/Amanda-Poshy-Fanpage


Post a Comment