Venezuela yatoa picha za rais Chaves
Serikali ya Venezuela imechapisha picha za mwanzo za rais wa taifa hilo
Hugo Chaves anaekabiliwa na ugonjwa wa saratani tangu afanyiwe upasuaji
mjini Havana, nchini Cuba miezi miwili iliyopita.
Taarifa mbalimbali zilisema rais huyo wa kisoshalisti, Hugo Chaves ana
shida ya kupumua na kwamba anapumua kutumua vifaa maalumu na akiwa na
shida ya kupumua. Picha hizi zilizotolewa sasa zinaonamuonesha kiongozi
huyo mwenye umri wa miaka 58 akitabasamu lakini sura yake ikiwa kama
imevimba. Alikuwa amelala kaitika kitanda cha hosiptali huku mabinti
wake wawili wakiwa pembeni na mwenyewe akisoma gazeti la serikali la
Cuba Granma.Maelezo kuhusu Chaves
Chavez hakuonekana hadharani, na mpaka sasa halijasikiwa lolote kutoka kwake tangu alipofanyiwa upasuaji wa nne uliyotokana na ugonjwa wa saratani Desemba 11, mwaka jana. Hata hivyo mpaka sasa sio picha hizo wala kutolewa taarifa madhubuti inayoweza kuonesha kama kiongozi huyo anaweza kurudi nyumbani au kulazimika kujiuzulu.
Makamu wa rais wa Venezuela ambae ndie anaekaimu nafasi ya urais Nicolas Maduro, alinukuliwa na vyombo vya habari hivi karibuni akisema rais Chaves yupo katika wakati mgumu sana ingawa hakutoa maelezo yoyote.

Post a Comment