ad

ad

RIHANNA ASHUTUMIWA KUVUNJA PENZI LA JUSTIN BIEBER

JUSTIN BIEBER ‘ametoka’ na Rihanna, limeandika jarida la kila wiki la Life & Style, ambalo limedai kuwa jambo hilo ndiyo sababu ya kweli nyuma ya kuachana na mpenzi wake Selena Gomez.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Gomez alimpiga chini Bieber Desemba mwaka jana baada ya kusikia habari za kushtua kwamba ‘amemchukua’ Rihanna.

Aliyeitwa ‘rafiki’ wa wenza hao wa zamani, amelieleza jarida hilo kuwa, “Justin ‘alifanya yake’ na Rihanna Februari mwaka juzi –wakati huo akiwa na miaka 16, huku tayari alikuwa amezama kwenye mapenzi na Selena.

Chanzo hicho kilisema kuwa, Bieber mwenye umri sawa na mdogo wa Rihanna, hakumweleza yeyote jambo hilo kwasababu lingemfanya aonekane kama ‘mbwa mchafu’.”

Kiliendelea kupasha kwamba ‘shoo’ hiyo ilifanyika nyumbani kwa Rihanna Los Angeles ama kwenye chumba cha hoteli ya Four Seasons, Beverly Hills, ambako Bieber anapendelea kukaa.

Chanzo kingine cha jarida hilo kilisema Bieber na Rihanna waliendeleza ‘kupeana raha’ wakati wa” walipokuwa wanachukua picha za viedo za Victoria’s Secret Fashion Show mwezi November.
Life & Style imetonywa kuwa, “Wakati wa mapumziko, walikwenda Hotel Giraffe. Walikuwa peke yao — walinzi wao walihakikisha hili. Mfanyakazi wa hoteli alizuia floo nzima kwaajili yao.”
Rihanna na Bieber, wote wawili wamekanusha jambo hilo
Via saluti5
Powered by Blogger.