ad

ad

Ukatili wa kijinsia sokoni wazidi kuwatesa wanawake

ASASI zinazotetea ukatili wa kijinsia, zimeshauriwa kutoa elimu kuhusiana na unyanyasaji kwa wanawake wengi zaidi sehemu za masoko ili kupunguza tatizo hilo kwa wajasiriamali hao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa kufungwa kwa mafunzo yaliyokuwa yanatolewa na asasi ya Equality for Growth (EfG) kuhusiana na kupinga ukatili kwa wanawake sokoni, kinamama hao walisema vitendo hivyo vimekithiri katika masoko.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika soko la Kigogo Sambusa, Mariam Rashid alisema kutolewa kwa mafunzo hayo sokoni kutachangia wanawake kujitambua na kutambua haki zao.

“Kabla ya mafunzo kutolewa tulikuwa tukinyanyasika sana, lakini hivi sasa wanaume sokoni hapa wamebadilika na kuacha kutumia lugha za matusi,”alisema Mariam.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake katika soko la Feri, Hamida Hindi alisema wanaume sokoni hapo walikuwa na tabia ya kuwadhalilisha kijinsia kwa kuwashikashika sehemu za miili yao bila ridhaa yao.
Alisema baadhi ya wanaume walikuwa wakikopa chakula lakini malipo ilikuwa shida, lakini mafunzo hayo yamewajengea ujasiri wanawake kudai fedha zao na hata kukataa mambo ya udhalilishaji.

Mtathmini Mradi wa EfG, Samora Julius alisema waliamua kuendesha mafunzo hayo katika masoko manne ya Halmashauri ya Ilala Dar es Salaam,ili kuweza kuondoa unyanyasaji huo.
Alisema mradi huo ambao umeyanufaisha masoko ya Ilala, Kigogo Sambusa, Buguruni na Kibasila,yamesaidia kuwafanya wanawake kujitambua katika shughuli zao.
“Tuliwafundisha jinsi ya kujiwekea akiba katika biashara zao,jambo ambalo limewasadia kwa kiasi kikubwa” alisema Julius.
Alisema hivi sasa wanawake katika masoko hayo wameweza kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa,ambavyo wamekuwa wakivitumia kusaidiana pale wanapokwama katika shughuli zao.
Powered by Blogger.